Pata taarifa kuu
UFILIPINO-TYPHOON HAIYAN

Misaada zaidi yawasili nchini Ufilipino wakati huu watu waliopoteza maisha wakizikwa kwenye kaburi la pamoja

Mamia ya miili ya watu waliopoteza maisha kutokana na kimbunga cha Typhoon Haiyan nchini Ufilipino hii leo wameanza kuzikwa kwenye kaburi la pamoja wakati huu ambapo maelfu ya raia walionusurika wakihitaji msaada zaidi wa kibinadamu.

Wanajeshi wa Ufilipino wakijaribu kuwaongoza mamia ya wananchi ambao wanahitaji msaada
Wanajeshi wa Ufilipino wakijaribu kuwaongoza mamia ya wananchi ambao wanahitaji msaada Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wakati miili hiyo ikizikwa zoezi la kutafuta miili zaidi linaendelea wakati huu ambapo bado vikosi vya uokoaji vimeendelea kupata miili ya watu ambao wamefukiwa kwenye matope na maporomoko ya udongo.

Maelfu ya raia wameendelea kufurika kwenye vituo vya kutoa misaada ya chakula huku wengi wakieleza kutokula kwa zaidi ya siku nne kutokana na kutofikiwa na wafanyakazi wa mashirika ya misaada.

Ndege kubwa ya jeshi la wanamaji wa Marekani inatarajiwa kuwasili hii leo ikiwa na wanajeshi zaidi ya elfu 5 pamoja na vyakula vya misaada kuongeza kasi ya kuwafikia maelfu ya wananchi ambao wanahitaji msaada.

Mkuu wa tume ya misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Valerie Amos ambaye amepiga kambi nchini Ufilipino ametembelea mji wa Tacloban ambao ndio umeathirika pakibwa kutokana na kimbunga hicho na kutoa wito wa misaada zaidi kuongezwa.

Bi Amos ameongeza licha ya wito wa muda mrefu kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada zaidi, bado zoezi hili halijafanikiwa vya kutosha kutokana na misaada mingi kuchelewa kuwafikia wahusika na kwa wakati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.