Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-HAMAS

Wawakilishi wa Palestina waonya kuwa wataondoka Cairo ikiwa wenzao wa Israel hawatatokea

Wawakilishi wa Palestina kwenye mazungumzo ya kusaka amani baina ya Hamas na Israel wameonya kuwa wataondoka Cairo leo Jumapili ikiwa wenzao wa Israel hawataonekana kwa ajili ya mazungumzo ya kusitisha mapigano baada ya Israel kufanya mashambulizi mapya ya anga huko Gaza na kuua Wapalestina zaidi ya tisa.

Moshi mzito ukifuka baada ya shambulizi la anga kutekelezwa na Israel huko Gaza 09 Agosti, 2014.
Moshi mzito ukifuka baada ya shambulizi la anga kutekelezwa na Israel huko Gaza 09 Agosti, 2014. REUTERS/Suhaib Salem
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya kusitisha mapigano huko Gaza yanatarajiwa kuanza hii leo jijini Cairo na ujumbe wa Israel unatarajiwa kuwasili leo,wakati wawakilishi wa Palestina na wapatanishi wa Misri wanawasubiri.

Lakini afisa wa Israel ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa mazungumzo hayawezi kufanyika mpaka Palestina isitishe kurusha makombora.

Wanamgambo wa Hamas walirusha makombora 25 kwa Israel jana Jumamosi, huku wito wa kusitisha mashambulizi ukizidi kutolewa ili kukomesha mauji ya raia waso na hatia ambapo tangu kuanza kwa mashambulizi hayo , karibu wapalestina elfu 2 wameuawa pamoja na waisrael 67 wengi wao wakiwa wanajeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.