Pata taarifa kuu
IRAQ-SYRIE-UTURUKI-KOBANE-ISIL-Usalama

Iraq: Wapeshmerga watumwa Kobane

Wapiganaji wa Kikurdi wa Iraq (Peshmerga), wametumwa kusaidia kundi la wapiganaji wa kikurdi kutoka Syria YPG linaloendesha vita dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam katika mji wa Kobane.

Wapiganaji wa Kikurdi wa Iraq (Pershmerga), Sptemba 8 mwaka 2014.
Wapiganaji wa Kikurdi wa Iraq (Pershmerga), Sptemba 8 mwaka 2014. REUTERS/Ahmed Jadallah
Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo umetolewa Jumatano Oktoba 22 na Bunge la eneo linalojitenga la Kurdistan nchini Iraq.

Wapiganaji hao wa Kikurdi wa Iraq watashirikiana na ndugu zao wa Syria kwa kuwatimua wapiganaji wa Doala la Kiislam ambao wanadhibiti baadhi ya maeneo ya mji wa Kobane kaskazini mwa Syria, licha ya mashambulizi yanayoendeshwa na muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani.

Wapiganaji hao wa Kikurdi wa Iraq walikua wakisubiriwa kuwasili katika mji wa Kobane tangu Jumapili Oktoba 19 mwaka 2014. Uamzi wa Bunge la Wakurdi nchini Iraq ndio umepelekea sasa wapiganaji hao wa kikurdi wa Iraq kujielekeza katika mji wa Kobane.

Kwa mujibu wa waziri wa eneo hilo linalojitegemea la Kurdistan nchini Iraq, wameamua kutuma idadi ndogo ya wapiganaji lakini wakiwa na vifaa vya kutosha kijeshi.. Hakuna taarifa zaidi ziliyotolewa lakini uamzi huo umechukuliwa sambamba na ombi la Wakurdi wa Kobane nchini Syria.

Wampiganaji wa Kikurdi katika mji wa Kobane wanaendelea na vita dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam, licha ya kuwa bado wanatumia bunduki za aina ya kalachnikov ambazo zimepitwa na wakati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.