Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI-NATO-TALIBAN-Usalaama-Siasa

Hali ya usalama yaendelea kudorora Afghanistan

Kundi la wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan, wametekeleza shambulio la bomu kwenye hoteli moja inayofikiwa na raia wa kigeni, saa chache baada ya mtu mmoja kujitoa muhanga akilenga ubalozi wa Uingereza mjini Kabul.

Viongozi wa usalama nchini Afghanistan wakionyesha silaha na risasi vilivyotumiwa na wapigaanji wa taliban katika shambulio dhidi ya hoteli moja ya kifahari mjini Kabul.
Viongozi wa usalama nchini Afghanistan wakionyesha silaha na risasi vilivyotumiwa na wapigaanji wa taliban katika shambulio dhidi ya hoteli moja ya kifahari mjini Kabul. REUTERS/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Watu sita wamethibitishwa kufa kwenye mashambulizi haya mawili akiwemo mwanajeshi mmoja wa Uingereza, katika shambulio ambalo ni muendelezo wa mashambulizi yanayofanywa na kundi la Taliban dhidi ya wageni na vikosi vya kimataifa.

Vikosi vya usalama nchini Afghanistan vimeendelea kukabiliwa na changamoto kubwa ya kudhibiti usalama nchini humo hasa baada ya kupungua kwa askari wa vikosi vya kimataifa ambao baadhi ya nchi zimeanza kuwaondoa wanajeshi wake ikiwemo Uingereza na Marekani.

Toka kuanza kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani waliokuwa wakiongoza operesheni za majeshi ya nchi za kujihami za magharibi NATO, wanamgambo wa Taliban wamezidisha mashambulizi wakiwalenga polisi na balozi za mataifa ya magharibi.

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa kwa sasa bado hali ya usalama nchini Afghanistan itasalia kuwa tete licha ya kuwepo kwa serikali mpya madarakani kwa kile wanachodai hakuna mpangilio mzuri wa serikali kuhakikisha wanajeshi wake wanakuwa na uwezo wa kusimamia usalama wakati huu wanajeshi wa NATO wakipungua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.