Pata taarifa kuu
JORDAN-IS-SYRIA-UGAIDI-USALAMA

Jordan yathibitisha kukamatwa kwa rubani wake na IS

Jordan imethibitisha kuwa rubani wa ndege ya kijeshi kutoka nchi hiyo amezuiliwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kislam, kaskazini mwa Syria.

Familia ya rubani wa ndege ya kijeshi ya Jordan yaiomba IS kumuonea huruma mwanao.Picha ya  Desemba 24 mwaka 2014 katika mji wa Karak, Jordan, mji ambao alizaliwa rubani huyo aliyekamakwa na IS.
Familia ya rubani wa ndege ya kijeshi ya Jordan yaiomba IS kumuonea huruma mwanao.Picha ya Desemba 24 mwaka 2014 katika mji wa Karak, Jordan, mji ambao alizaliwa rubani huyo aliyekamakwa na IS. REUTERS/Muhammad Hamed
Matangazo ya kibiashara

Rubani huyo amekua akiendesha mashambulizi ya anga nchini Syria kwa niaba ya muungano wa kimataifa unoongozwa na Marekani katika vita dhidi ya kundi la wapigaanji wa Dola la Kiislam.

Kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam limesthibitisha kuwa limeidungua ndege hiyo kwa kombora, lakini Idara ya ujasusi ya Marekani imekanusha taarifa hiyo, na kubaini kwamba wanajihadi hao hawakudungua ndege hiyo yenye chapa F 16, blia hata hivyo kutoa maelezo zaidi. taarifa hii ya kudunguliwa kwa ndege hiyo kumeiweka Jordan katika nafasi ngumu.

Picha ambazo zilikua zikiwekwa hewani jumtano Desemba 24 kwenye mitandawo tofauti duniani zilionesha mtu akivalia T-shirt nyeupe, huku akizungukwa na wapiganaji wenye silaha. Picha zingine zilionyesha mabaki ya ndege ambayo inadaiwa kuwa yalikua mabaki ya ndege ya Jordan, ambayo haikurejea baada ya kutekeleza wajibu wake katika anga ya Syria katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam Jumatano Desemba 24.

Jordan ni moja ya nchi za kiarabu ziliyokubali kushiriki katika operesheni ya muungano wa kimataifa unaoongozwa na Marekani dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. Saudia Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrein na Qatar ni miongoni mwa nchi hizo za kiarabu zinazoshiriki katika operesheni hiyo. Majeshi ya nchi hizo yanaendesha mara kwa mara operesheni hiyo nchini Iraq na Syria, ambapo kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam wanaendesha harakati zake.

Awali Jordan ilisisitiza kuwa ndege yake ilianguka katika mazingira ya kawaida, wakati ambapo kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam lilikiri kuidungua ndege hiyo kwa kombora.

Ni kwa mara ya kwanza mwanajeshi wa vikosi vya muungano wa kimataifa dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam kukamatwa na wapiganaji wa kundi hilo. Baba wa rubani huyo wa Jordan ametolea wito kundi la wapiganaji wa Dola la kiislam “kumsamehe” mwanaye.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.