Pata taarifa kuu
Yemen-Mapigano

Waasi wa Kishia nchini Yemen wasonga mbele kwenye uwanja wa mapigano

Waasi wa Yemeni wameendelea kupata mafanikio mapya ya kusonga mbele katika mapambano yanayoendelea katika mji wa Aden kusini mwa nchi hiyo ambayo inakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vyenye muelekeo wa kimadhehebu

Wapiganaji wa kishia wa kundi la houthis mjini Aden, Jumamosi April 4.
Wapiganaji wa kishia wa kundi la houthis mjini Aden, Jumamosi April 4. AFP PHOTO / SALEH AL-OBEIDI
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati huu majeshi ya pamoja yanayoongozwa na Saudi Arabia yakiendeleza mashambulizi dhidi ya waasi hao huku ukitolewa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi ya anga ili kupisha usambazaji wa misaada ya kibinadamu.

Katika mji wa Aden waasi hao wa kishia wameendelea kusonga mbele katika wilaya ya Mualla na kuteka makao makuu ya serikali ya jimbo.

Shirika la Msalaba mwekundu nchini Yemeni limetoa wito huo ili kuwawezesha wananchi na familia zao kutafuta mahaitaji hayo ya kibinadamu kama vile maji, chakula na misaada ya matibabu.

Katika hatua nyingine Urussi mwishoni mwa juma imewasilisha azimio mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa la kuzitaka pande zinazopambana kusitisha mapigano ili misaada ya kibinadamu iweze kuwafikia wahitaji.

Mashambulizi ya anga yanayoongozwa Saudi Arabia dhidi ya wapiganaji wa waasi wa kishia yameingia katika siku ya kumi na mbili majeshi hayo yakikabaliana na waasi hao usiku na mchana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.