Pata taarifa kuu
SYRIA-UN-MSAADA

Msaada wa kibinadamu wasubiriwa Syria

Msafara wa magari yanayobeba msaada wa kibinadamu unatazamiwa kuwasili Jumatano hii katika miji kadhaa nchini Syria inayoendelea kuzingirwa waasi pamoja na majeshi ya Syria.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura katika mkutano na waandishi wa habari mjini Damascus, Februari 16, 2016.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura katika mkutano na waandishi wa habari mjini Damascus, Februari 16, 2016. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati hio huo Uturuki imetoa wito kwa kuingilia kati kwa majeshi yake ya nchi kavu na yale ya washirika wake, hivyo kukwamisha mkataba wa usitishwaji wa mapiganoambao unelianza kutekelezwa wiki hii.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura, aliwasili Jumatatu katika mji mkuu wa Syria Damascus, alipata ruhusa kutoka kwa serikali ya Syria kupeleka msaada katika miji kadhaa ambapo watu wanaishi katika hali mbaya.

"Kesho (Jumatano) tutatahmini (nia ya kuachia msaada upite) na tutakua na uwezo wa kuzungumza zaidi baadae," amesema mjumbe wa Umoja wa Mataifa ambaye alikutana mara mbili na Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Walid Muallem.

Kwa mujibu wa msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Msaada wa Kibinadamu (OCHA), maeneo saba yanayozingirwa na majeshi ya serikali au waasi yanapaswa kupatishiwa msaada katika siku zijazo. Maeneo haya ni pamoja na "Deir Ezzor, Foua, Kafraya katika jimbo la Idleb, Madaya, Zabadani, Kafar Batna na Mouadamiyat al-Sham", ameongeza msemaji wa OCHA.

Kwa mujibu wa chanzo cha shirika la Msalaba Mwekundu nchini Syria, msaada wa Jumatano utaelekezwa maeneo yanayokaliwa na Mashia wengi ya Foua na Kafraya, yanayozingirwa Kaskazini na waasi, pamoja na Madaya na Zabadani, yanayozingirwa na jeshi katika jimbo la Damascus.

Hata hivyo mapigano bado yanaendelea kurindima katika maeneo mbalimbali nchini Syria. Jumanne usiku, watu wasiopungua watano waliuawa katika mashambulizi ya muungano wa kimataifa unaongozwa na Marekani dhidi ya mji Kaskazini Mashariki mwa Syria unaodhibitiwa na kundi la Islamic State IS, kwa mujibu wa shirika la Haki za binadamu nchini Syria (OSDH).

Ufaransa, Uingereza, lakini pia, Uholanzi na Uturuki ni sehemu ya muungano huu unaopambana na kundi la IS kwa mashambulizi ya anga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.