Pata taarifa kuu
SYRIA-UN-MAPIGANO

Syria: UN yawaondoa raia na majeruhi 500 katika miji 4 inayozingirwa

Nchini Syria, Umoja wa Mataifa, Jumatano hii, umewaondoa watu 500 ikiwa ni pamoja na wagonjwa au majeruhi na familia zao kutoka miji kadhaa inayozingirwa na vikosi vya serikali au na waasi.

Wakazi wa Zabadani, mji unaozingirwa na vikosi vya serikali, wakisubiri kuhamishwa, Jumatano hii, Aprili 20, 2016.
Wakazi wa Zabadani, mji unaozingirwa na vikosi vya serikali, wakisubiri kuhamishwa, Jumatano hii, Aprili 20, 2016. REUTERS/via Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kutiwa wasiwasi juu ya hatima ya raia 40,000 wa Syria waliokimbia katika jimbo la Aleppo hivi karibuni.

Watu mia mbili na hamsini, raia na wapiganaji, waliojeruhiwa au wagonjwa watahamishwa kutoka maeneo yanayokaliwa na Mashia wengi ya Foua Kfarya, yanayozingirwa na waasi katika jimbo la Idleb, kaskazini mwa Syria. Idadi kama hiyo itahamishwa kutoka miji inayokaliwa na Wasuni ya Zabadani na Madaya, inayozingirwa na jeshi la Syria na washirika wake, karibu na mpaka wa Lebanon.

Operesheni hii kababmbe ya kibinadamu, iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa, inaendeshwa na timu za Umoja wa Mataifa, Shirika la Msalaba Mwekundi kutoka Syria na Shirika la Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC).

Hatua ya kwanza ya mpango huo ilikumbwa na tukio la ajabu. Msafara wa Shirika la Msalaba Mwekundu kutoka Syria, ambao ulikuwa ukijianda kuingia katika eneo la Madaya, uligeuza na kurudi nyuma baada ya kushambuliwa kwa risasi zilizorushwa kutoka katika mji huo.

Baada ya masaa machache, shughuli iliendelea tena vizuri. Operesheni hii inatarajiwa kukamilika Alhamisi hii. Wagonjwa na majeruhi watatibiwa katika hospitali za Damascus na mji wa Idleb, unaodhibitiwa na waasi wa kundi la Al-Nosra Front, tawi la al-Qaida nchini Syria.

Katika eneo la Doumeir, kaskazini mwa mji wa Damascus, waasi wa kundi hili walitangaza kujiunga na kundi la Islamic State (IS), waliondoka katika mji huo na familia zao. Kuondoka kwao kulikuja baada ya upatanishi ulioendeshwa na watu mashuhuri wa mji huo, ili kuzuia mashambulizi ya jeshi la Syria.

■ Wasyria elfu arobaini wakimbia mji wa Aleppo

Umoja wa Mataifa umetangaza kutiwa wasiwasi juu ya hatima ya zaidi ya raia 40,000 wa Syria waliokimbia mji wa Aleppo, ambako mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi yanaendelea licha ya mkataba wa kusitisha mapigano ulioafikiwa tangu mwishoni mwa mwezi Februari. Wakati ambapo mjini Geneva mazungumzo ya amani yanakwenda kwa mwendo wa kinyonga baada ya kuondoka kwa idadi kubwa ya wajumbe wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.