Pata taarifa kuu

Iran yaahidi jibu 'kali' na 'mbaya' endapo Israel italipiza kisasi

Rais wa Iran Ebrahim Raïssi ameonya kwamba "hatua ndogo" ya Israel dhidi ya "maslahi ya Iran" itaibua "jibu kali" kutoka kwa nchi yake, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyochapishwa Jumanne hii, Aprili 16 na ofisi ya rais.

Rais wa Iran, Ebrahim Raïssi, pia kwa mara nyingine tena ameshutumu "uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Magharibi kwa utawala wa Kizayuni", ambao ni "sababu ya mvutano katika ukanda", kulingana na taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.
Rais wa Iran, Ebrahim Raïssi, pia kwa mara nyingine tena ameshutumu "uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Magharibi kwa utawala wa Kizayuni", ambao ni "sababu ya mvutano katika ukanda", kulingana na taarifa hiyo kwa vyombo vya habari. © AP
Matangazo ya kibiashara

Kama ukumbusho, Israel, kupitia msemaji wa jeshi, iliahidi "jibu" kwa shambulio kubwa na ambalo halijawahi kutokea lililozinduliwa na Iran usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili kwenye ardhi ya Israeli.

"Sasa tunatangaza kwa uthabiti kwamba hatua ndogo dhidi ya maslahi ya Iran hakika itasababisha jibu kali, pana na mbaya dhidi ya wahusika wake wote," Ebrahim Raïssi amesema katika mazungumzo ya simu na Amir wa Qatar Tamim bin Hamad Al-Thani mapema siku yaJumatatu.

"Haki ya kujilinda"

Rais wa Irani ameonyesha kuwa nchi yake ililenga mwishoni mwa wiki hii, "kwa kutumia haki yake ya kujilinda", "vituo" ambapo shambulio la bomu, lililohusishwa na Israeli, la ubalozi wa Iran lilipangwa , Aprili 1.

Operesheni hii ambayo haijawahi kushuhudiwa "ilifanywa kwa mafanikio kwa lengo la kumuadhibu mchokozi," ameongeza.

Ebrahim Raïssi pia kwa mara nyingine tena ameshutumu "uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Magharibi kwa utawala wa Kizayuni", ambao ni "sababu ya mvutano katika ukanda", kulingana na taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.

Siku ya Jumatatu jioni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Ali Bagheri alionya mamlaka ya Israel kupitia televisheni ya taifa kwamba, katika tukio la jibu, "italazimika kutarajia pigo kali na kubwa zaidi, lenye kasi na la haraka zaidi" kutoka kwa upande wa Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.