Pata taarifa kuu

UN: Israel yapaswa kuacha kuunga mkono' ghasia za walowezi katika Ukingo wa Magharibi

Vikosi vya Israel lazima "vikome mara moja ushiriki wao kikamilifu na uungaji mkono" katika mashambulizi ya walowezi dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu huko Geneva imesema leo Jumanne.

Mmoja wa walowezi wa Kiisraeli akisali katika kituo cha Ukingo wa Magharibi cha Amona mnamo Desemba 18, 2016.
Mmoja wa walowezi wa Kiisraeli akisali katika kituo cha Ukingo wa Magharibi cha Amona mnamo Desemba 18, 2016. REUTERS/Baz Ratner
Matangazo ya kibiashara

"Mamlaka za Israel badala yake zinapaswa kuzuia mashambulizi zaidi, hasa kwa kuwawajibisha wale wanaohusika," amesema msemaji wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu, Ravina Shamdasani, wakati wa mkutano wa kila siku wa Umoja wa Mataifa huko Geneva.

Wakati huo huo, jeshi la Israel limesema leo Jumanne asubuhi kwamba limeendeleza mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Gaza katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita. "Wanajeshi wa Israel waliendelea kufanya kazi katikati mwa Ukanda wa Gaza, vifaru viliua idadi kubwa ya magaidi waliotambuliwa ambao walikuwa wakiwakabili," jeshi liliwasiliana kwenye ujumbe wa Telegram katika muhtasari wa kila siku.

Israel ilikuwa imethibitisha kwamba shambulio la Iran halitabadilidha malengo yake dhidi ya Hamas, mshirika wa Iran, shabaha ya mashambulizi yake yaliyotekelezwa kwa zaidi ya miezi sita katika ardhi ya Palestina. Shambulizi hili limesababisha vifo vya watu 33,797, kulingana na wizara ya afya ya Ukanda wa Gaza inayosimamiwa na Hamas. Katika saa ishirini na nne, vifo vya ziada 68 vimerekodiwa, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa wizara ya Afya , ambayo pia imeripoti majeruhi 76,465 kufikia sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.