Pata taarifa kuu

Iran kujibu vikali iwapo Israeli italipiza kisasi shambulio la wikendi iliopita

Rais wa Iran Ebrahim Raisi ameonya kuwa hatua ya Israeli kutekeleza shambulio la kulipiza kisasi itajibiwa vikali, onyo linalokuja wakati huu eneo la Mashariki ya kati likikabiliwa na hofu kuwa Israeli itajibu shambulio la Iran la wikendi iliopita.

Mifumo ya ulinzi wa angani ya Israeli wakati wa shambulio la Iran kuelekea nchini Israeli. 14 avril 2024.
Mifumo ya ulinzi wa angani ya Israeli wakati wa shambulio la Iran kuelekea nchini Israeli. 14 avril 2024. © Amir Cohen / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Ebrahim Raisi ametoa onyo hilo wakati wa gwaride la kila mwaka la jeshi ambalo limefanyika Jumatano katika  kambi ya kaskazini mwa mji mkuu, Tehran, kutoka eneo lake la kawaida kwenye barabara kuu kusini mwa mji huo.

Iranian President Ebrahim Raisi attends a meeting with Russian President Vladimir Putin in Moscow, Russia December 7, 2023
Rais wa Iran Ebrahim Raisi wakati wa mkutano na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow, Urusi Desemba 7, 2023 via REUTERS - SPUTNIK

Mamlaka ya Irani haikutoa maelezo ya kina kuhusu kuhamishwa kwa eneo la gwaride hilo, ambapo pia televisheni ya serikali haikuitangaza moja kwa moja, kama ilivyokuwa kwa miaka iliyopita.

Iran ilirusha mamia ya makombora na ndege zisizo na rubani kuelekea Israeli mwishoni mwa juma kujibu shambulio la Israeli kwenye jumba la ubalozi wa Iran nchini Syria mnamo Aprili 1 na kuua watu 12, wakiwemo majenerali wawili wa jeshi la Iran.

Soma piaIran yarusha ndege zisizo na rubani na makombora zaidi ya 200 dhidi ya Israel

Israel, kwa usaidizi kutoka Marekani, Uingereza, nchi jirani ya Jordan na mataifa mengine, ilifanikiwa kuzuia takriban makombora yote na ndege zisizo na rubani za Iran.

Israel imeapa kujibu shambulio hilo, bila kusema ni lini au vipi, huku washirika wake wakitoa wito kwa pande zote kuepuka kuchochea mzozo zaidi katika Ukanda wa Mashairki ya kati.

Waandamanaji nchini Iran wakisherehekea shambulio la nchi yao dhidi ya Israeli mnamo Aprili 14, 2024 huko Tehran.
Waandamanaji nchini Iran wakisherehekea shambulio la nchi yao dhidi ya Israeli mnamo Aprili 14, 2024 huko Tehran. AFP - ATTA KENARE

Raisi alisema shambulio la Jumamosi lilikuwa dogo, na kwamba kama Iran ingetaka kufanya shambulio kubwa zaidi, "hakuna kitakachosalia kutoka kwa kile alichokitaja kama utawala wa Kizayuni." Kama alivyonukuliwa na shirika rasmi la habari la IRNA.

Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia al-Sudani naye anasema alimshinikiza Rais Joe Biden kuhusu kuwepo kwa hali ya utulivu Mashariki ya kati, hatua inayokuja wakati huu ikihofiwa  kuwa mzozo huo unaweza kuwa mbaya zaidi kati ya Iran na mshirika wa Marekani Israel.

Soma piaJapan yaitaka Iran 'kujizuia' baada ya kuishambulia Israel

Al-Sudani alizungumza na waandishi wa habari Jumanne usiku akiwa katika ziara jijini Washington ambapo amefanya mazungumzo na rais Biden katika Ikulu ya White House Jumatatu.

Hillary Ingati-RFI-Kiswahili/AP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.