Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa waomba msaada wa dola bilioni 2.8 kwa Gaza

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anabaini kwamba Israel inafanya "kila linalowezekana" kuboresha hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza. Waziri Mkuu wa Israel "anakanusha madai ya mashirika ya kimataifa kuhusu njaa" katika eneo la Palestina. Umoja wa Mataifa (UN) unabaini kwamba kuna "hatari kubwa ya njaa" huko Gaza. Mashirika ya kimataifa na mashirka yasiyo ya kiserikali yanaomba dola bilioni 2.8 kufadhili shughuli zao katika Ukanda wa Gaza.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameitisha mkutano wa kila wiki wa baraza la mawaziri katika Wizara ya Ulinzi huko Tel Aviv, Israel, Januari 7, 2024.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameitisha mkutano wa kila wiki wa baraza la mawaziri katika Wizara ya Ulinzi huko Tel Aviv, Israel, Januari 7, 2024. © Ronen Zvulun / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na wanahabari wetu mjini Jerusalem, Nicolas Benita na Guilhem Delteil

Dola bilioni 2.8 ni pesa nyingi sana,anakiri mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) katika Maeneo ya Palestina. Lakini leo, huko Gaza, tunapaswa kutunza watu kutoka asubuhi hadi jioni, anasisitiza Andrea de Domenico:

"Lazima ufikirie juu ya siku ya kawaida kwa kila mmoja wetu, unapoamka hadi wakati wa kulala, na ufikirie kuwa yote hayo hayapatikani leo. Na hivyo, kuna lazima kuwe na msaada wa kuwapa, kutoka kwa mswaki na maji hadi blanketi tunapoenda kulala usiku, vyoo, nk. Vyote. "

Fedha hizi ni zaidi ya mara tano zaidi ya zile zilizoombwa miaka iliyopita. Lakini inabakia chini ya mahitaji muhimu. Kwa kweli itachukua angalau bilioni moja zaidi. Hata hivyo, mashirika ya yanayotoa misada ya kibinadamu yanawekewa mipaka na hali ambayo yanafanya kazi leo huko Gaza.

"Ili kufanya kazi, shirika lolote linahitaji ofisi, kompyuta, umeme, maji, chakula cha kulisha wafanyakazi wanaofanya kazi, mafuta ya kuendesha shughuli mbalimbali katika ukanda a Gaza, hususan kusafiri na bidhaa zote ili kutoa msaada. Yote haya yanasalia kuwa changamoto kubwa,” anakumbusha Andrea de Domenico.

Maadamu vita vinaendelea na vikwazo vya uagizaji bidhaa kutoka nje vimesalia kuwa vikali, wahusika wa misaada ya kibinadamu hawataweza kukidhi kikamilifu mahitaji ya Wagaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.