Pata taarifa kuu

Iran: Rais wa Iran Ebrahim Raïssi kuzuru Pakistan kwa siku tatu

Rais wa Iran Ebrahim Raïssi anatarajiwa nchini Pakistan kuanzia Jumatatu Aprili 22 hadi Jumatano Aprili 24. Hii ni ziara yake ya kwanza baada ya kuzuka kwa mvutano mfupi kati ya majirani hao wawili Januari 2024.

Rais wa Iran Ebrahim Raïssi akitoa hotuba wakati wa sherehe za gwaride la Siku ya Jeshi la taifa huko Tehran, Iran, Aprili 17, 2024.
Rais wa Iran Ebrahim Raïssi akitoa hotuba wakati wa sherehe za gwaride la Siku ya Jeshi la taifa huko Tehran, Iran, Aprili 17, 2024. © Majid Asgaripour / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Tehran, Siavosh Ghazi

Ebrahim Raïssi, akiandamana na mawaziri na wafanyabiashara kadhaa, anatarajiwa kukutana na rais na waziri mkuu wa Pakistan. Pia atatembelea Lahore, mashariki mwa Pakistan, na Karachi, jiji kubwa la pwani ya kusini.

Tehran na Islamabad zinaongeza ishara za utulivu baada ya uhusiano wao kuzorota ghafla, wakati Iran ilipofanya shambulio la kombora na ndege zisizo na rubani mnamo Januari 16 dhidi ya kundi la "kigaidi" katika ardhi ya Pakistan. Pakistan ilijibu siku mbili baadaye kwa kulenga "maficho ya magaidi" nchini Iran. Baada ya siku chache za kutoelewana, nchi hizo mbili hatimaye zilitangaza kurejea katika hali ya kawaida ya uhusiano wao.

Mwanzoni mwa mwezi  huu wa Aprili, karibu wanachama ishirini wa vikosi vya usalama vya Iran waliuawa kusini-mashariki, mpakani mwa Pakistan na Afghanistan, na kundi la wanajihadi lililoko Pakistan, kulingana na mamlaka ya Iran.

Pakistan pia ilitangaza kuanzisha tena mradi mkubwa wa kujenga bomba la gesi la kusambaza gesi ya Iran kwa Pakistan, licha ya upinzani kutoka kwa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.