Pata taarifa kuu
London

Muamba awatambua na kuzungumza na familia yake

Fabrice Muamba mchezaji wa klabu ya soka ya Bolton nchini Uingereza ameanza kupata nafuu lakini hali yake haijawa nzuri sana,na madaktari wake wanasema bado amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali wa moyo jijini London.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo,Muamba ameweza kuwatambua familia yake na kujibu maswali kadhaa kutoka kwao,na pia amenyanyua mguu wake.

Madaktari wake  wanasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 sasa anaweza kupumua bila ya msaada mashine.

Muamba alizimia Jumamosi iliyopita wakati wa mchuano kati ya klabu yake ya Boston na Tottenham Hotspurs katika kinyanganyiro cha kuwani taji la FA.

Muamba ni mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokarasia ya Kongo na alihamia  nchini Uingereza na kujiunga na klabu ya vijana chipukizi ya Arsenal.

Amekuwa akiichezea timu ya taifa ya Uingereza katika mashindano kadhaa ya chipukizi tangu mwaka 2007 na amecheza zaidi ya mara thelathini.

Muamba pia amewahi kuichezea klabu ya Birmighham kabla ya kujiunga na Bolton Wanderes.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.