Pata taarifa kuu
Uingereza

Manchester City wafufua matumaini ya kushinda ligi kuu ya soka nchini Uingereza

Manchester City imefufua matumaini ya kunyakua taji la soka la klabu bingwa nchini Uingereza baada ya kuishinda Chelsea mabao 2 kwa 1 katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad Jumatano usiku.

Matangazo ya kibiashara

Mshambulizi Carlos Tevez ambaye alirejea kuichezea klabu yake kwa mara ya kwanza tangu aliposimamishwa kuichezea timu  hiyo kwa sababu za kinidhamu kuanzia mwezi Septemba mwaka uliopita,alisaidia timu yake kupata bao la ushindi baada ya  kutoa pasi iliyomwezesha Samir Nasir kufunga bao la ushindi katika dakika za lala salama.

Vijana hao wa Roberto Mancini sasa wanasalia na alama moja kuwafikia viongozi wa ligi  Manchester United ambao wana alama 70.

Chelsea ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Garry Cahill kabla ya Sergio Aguero kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti baada ya Michael Essien kuunawa mpira.

Katika matokeo mengine,Arsenal imepanda hadi katika nafasi ya tatu kwa alama 55 baada ya kuishinda Everton bao 1 kwa 0.

Tottenham Hotsuprs ilitoka sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya Stoke City na imeshuka hadi katika nafasi ya nne alama moja chini ya Arsenal.

Queens Park Rangers nayo iliishangaza Liverpool kwa kuichabanga magoli 3 kwa 2 na kupanda hadi katika nafasi ya 17 kwa alama 25 katika msururu wa ligi hiyo.

Bolton Wanderes,Wigan na Wolves zinashikilia nafasi za mwisho kwa alama 23 na 22 mtawalia katika msururu wa ligi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.