Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Manchester City yaambulia kipigo mbele ya Arsenal huku Manchester United ikiweka tofauti ya pointi kufikia nane

Mbio za Ubingwa nchini Uingereza zinaanza kufikia ukongoni baada ya michezo miwili iliyopigwa jana kutoa matoke ambayo yanadhihirisha nguvu waliyokuwa nayo Manchester City imeanza kwisha mbele ya washindani wao Manchester United.

Kiungo wa Klabu ya Arsenal Mikel Arteta akishngilia baada ya kufunga goli la pekee kwenye mchezo wao dhidi ya Manchester City
Kiungo wa Klabu ya Arsenal Mikel Arteta akishngilia baada ya kufunga goli la pekee kwenye mchezo wao dhidi ya Manchester City
Matangazo ya kibiashara

Ushindi wa nyumbani wa Manchester United mbele ya Queens Park Rangers QPR wa magoli 2-0 huku Manchester City ikipata kipigo kingine mbele ya Washika Bunduki wa London Arsenal imefanya tofauti ya pointi kuwa nane baina ya timu hizo mbili.

Manchester City ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu hii imejikuta ikipoteza matumaini hayo baada ya kujikuta ikipata matokeo mabaya katika siku za hivi karibuni wakati wapinzani wao Manchester United wakionekana kuimarika zaidi.

Manchester City waliingia uwanjani jana huko Emirates huku wakiwa na matoketo ua ushindi wenye utata walioupata Manchester United kwa kuwafunga QPR nyumbani Old Trafford kabla ya Arsenal nao kupata ushindi uliowamaliza City.

Magoli ya kwake Wayne Rooney kupitia mkwaju wa penalti uliojaa utata mwingi na lile la Paul Scholes yaliwafanya Manchester United kujihakikishia kusalia kileleni kabla ya Arsenal kupata ushindi wa dakika za mwishoni kwa goli la Mikel Arteta.

Manchester City walilazimika kumaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya mshambuliaji wake mtukutu Mario Balotelli kulimwa kadi nyekundu huku Yaya Toure akishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kuumia goti kufuatia kugongana na Alex Song.

Kutokana na kitendo cha Balotelli kulimwa kadi nyekundu kocha wake Roberto Mancini amesema kuna uwezekano mkubwa akamuuza mshambuliji huyo ambaye kila kukicha amekuwa akiibuka na kituko kipya.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amewaonya wachezaji wake kutoridhika na ushindi huo badala yake amewataka kuangalia mchezo wao wa jumatano dhidi ya Wolves ili kuhakikisha wanafanikiwa kumaliza katika nafasi tatu za juu.

Timu zinazoshiliki kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza kila moja imesalia na michezo sita kabla ya kuhitimisha msimu wa mwaka huu huku nafasi ya Ubingwa ikiwa kwa klabu mbili ambazo ni Manchester United na Manchester City.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.