Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Mshambuliaji wa Manchester City Balotelli anatarajiwa kuzungumza na Uongozi juu ya mustakabali wake

Mshambuliji wa Kimataifa wa Italia anayekipiga katika Klabu ya Manchester City ambaye kwa sasa anaonekana ni mtukutu zaidi Mario Balotelli anatarajiwa kuzungumza na Uongozi wa Klabu yake juu ya mustakabali wake wa kuendelea kuwepo msimu ujao hapo Etihad au la.

Mshambuliji wa Klabu ya Manchester City Mario Balotelli anayetarajiwa kukutana na Uongozi wa Timu yake kujadili mustakabali wake
Mshambuliji wa Klabu ya Manchester City Mario Balotelli anayetarajiwa kukutana na Uongozi wa Timu yake kujadili mustakabali wake
Matangazo ya kibiashara

Balotelli ameingia matatani na Kocha wake Roberto Mancini baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo wao uliopigwa siku ya jumapili dhidi ya Arsenal baada ya kulimwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya beki Bacary Sagna.

Mancini alihojiwa na waandishi wa habari na kusema wazi kuwa hajui kama Balotelli ataendelea kuwepo msimu ujao kutokana na kuigharimu Klabu hiyo kutokana na tabia zake zinachochangia kulimwa kadi bila ya sababu za msingi.

Balotelli ameomba radhi kwa kitendo ambacho amekifanya cha kupewa kadi nyekundu kwa Uongozi wa Klabu hiyo akikiri ni kitendo ambacho hakikustahili kufanywa wakati timu inahangaika kupata goli la kusawazisha.

Licha ya kosa hilo la kupewa kadi nyekundu Balotelli alikuwa ni mwenye bahati kwani alicheza rafu mbaya kwa kiungo wa Arsenal Alex Song ambayo kama mwamuzi angeioa basi alikuwa anastahili kumtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.

Tayari Chama Cha Soka Nchini Uingereza FA kimeanza uchunguzi wa tukio hilo na iwapo atakutwa na hatia ya kulitekeleza ni wazi huenda akakabiliwa na adhabu zaidi kwa kosa hilo.

Tangu Balotelli ajiunge na Manchester City misimu miwili iliyopitwa ameshapewa kadi nne nyekundu huku pia akiwa na rekodi chafu ya matendo yake ikiwepo kupigana na baadhi ya wachezaji wenzake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.