Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Ligi Kuu Nchini Uingereza kuendelea wakati Wigan wakijiapiza kuwadhibiti Manchester United

Ligi Kuu nchini Uingereza inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi hii usiku wa jumatano ambapo michezo minne inatarajiwa kupigwa katika madimba tofauti wakati huu mbio za kusaka ubingwa zikizidi kushika kasi.

Kocha wa Wigan Athletic Roberto Martinez ambaye amesema wapo tayari kukabiliana na Manchester United
Kocha wa Wigan Athletic Roberto Martinez ambaye amesema wapo tayari kukabiliana na Manchester United
Matangazo ya kibiashara

Michezo hii inakuja baada ya hapo jana Vijogoo vya Jiji Klabu ya Liverpool kuvuna ushindi wa ugenini mbele ya Blackburn Rovers katika mchezo ulipigwa katika Uwanja wa Ewood Park kwa magoli 3-2.

Manchester United itasafiri kuwafuata Wigan Athletic wakati huu ambapo Kocha Roberto Martinez akisema wapo tayari kwa mchezo huu wakati huu wakipigana na baalaa la kushuka daraja linalowakabili.

Wigan wanashuka dimbani wakiwa wamepoteza michezo kumi na nne iliyotangulia kila wanapokabiliana na Manchester United huku Martinez akisema wanajivunia mchezo safi ambao walionesha kwenye michezo yao miwili kati ya Liverpool na Chelsea.

Manchester City nao watakuwa kibaruani kwenye dimba la nyumba la Etihad huku bado wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo dhidi ya Arsenal uliopigwa mwisho mwa juna na leo wanapambana na West Browich Albion.

Manchester City watakuwa na ahueni baada ya Chama Cha Soka Nchini Uingereza FA kusema hakitomuongezea adhabu Mario Balotelli kwa kitendo chake cha kumkanyaga Alex Song kwa kuwa mwamuzi Martin Atkinson kutoandika chochote kwenye ripoti yake.

Washika Bunduki wa Jiji la London Arsenal wenyewe watakabiliana na Wolves kwenye mchezo ambao watakuwa wanapigana kwa udi na uvumba ili kupata ushindi kujigakikishia kupata nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Mchezo mwigine utazikutanisha Queens Park Rangers dhidi ya Swansea mchezo ambao unatarajiwa kuwa ni wa upinzani mkubwa baina ya timu hizo ambayo kila moja itakuwa inasaka matokeo ya ushindi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.