Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Manchester United yapata kichapo kutoka kwa Wigan huku City ikishinda na kupunguza tofauti ya pointi

Heka heka za Ligi Kuu Nchini Uingereza zimefika patamu baada ya kupigwa michezo minne hapo jana na kushuhudia vinara Manchester United wakipoteza pointi tatu na hivyo tofauti ya pointi baina yao na Manchester City kusalia tano kutoka nane ilizokuwa awali mwishoni mwa juma.

Wachezaji wa Manchester United wakiwa hawana la kufanya baada ya kuambulia kichapo kwenye mchezo wao dhidi ya Wigan Athletic
Wachezaji wa Manchester United wakiwa hawana la kufanya baada ya kuambulia kichapo kwenye mchezo wao dhidi ya Wigan Athletic
Matangazo ya kibiashara

Manchester United ilipata kipigo cha kushtukia kutoka kwa Klabu inayopigana kutoshuka daraja ya Wigan Athletic baada ya kuchabangwa goli moja kwa nunge kwenye mchezo uliopigwa katika Dimba la DW.

Goli la Shaun Maloney la dakika hamsini ndilo lilisitisha rekodi nzuri ya Manchester United mbele ya Wigan ya kushinda michezo yao yote kumi na minne walipokutana awali kitu ambacho kimemchukiza Kocha Sir Alex Ferguson.

Kufungwa huko kulikuwa kuchungu zaidi baada ya mahasimu wao Manchester City kufanikiwa kupata ushindi wa magoli manne kwa bila mbele ya West Brom katika Uwanja wa Etihad na hivyo kupunguza tofauti ya pointi na kusalia tano.

Magoli mawili ya kwake Sergio Aguero huku mengine mawili yakifungwa na Carlos Tevez na Davis Silva yalitosha kuwapa ushindi siku tatu baada ya kushuhudia wakipoteza mchezo wao dhidi ya Arsenal huko Emirates.

Katika Mchezo mwingine Washika Bunduki wa Jiji las London Arsenal wameendeleza wimbi lao la ushindi baada ya kuifunga Wolves kwa magoli matatu kwa bila na kuendelea kujihakikishia kumaliza katika nafasi ya tatu.

Magoli ya Arsenal yalifungwa na Robin Van Persie kwa mkwaju wa penalty kabla ya Theo Walcott na Yossi Benayoun kufunga magoli mengine dhidi ya Wolves iliyomaliza ikiwa na wachezaji kumi baada ya Sebastian Bassong kupewa kadi nyekundu.

Katika Mchezo mwingine vijana wa Queens Park Rangers baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Manchester United mwishoni mwa juma jana walifanya vyema kwa kuwafunga Swansea kwa juma ya magoli matatu.

Kwa ushindi huo wa QPR inaendelea kupambana kujiepusha na balaa la kushuka daraja wakati huu ambapo michezo mitano imesalia kabla ya Msimu wa Ligi mwaka huu kufikia kikomo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.