Pata taarifa kuu
BAHRAIN

Mbio za langalanga zinazotarajiwa kufanyika nchini Bahrain hatarini kutofanyika

Maelfu ya wananchi wakiongozwa na wanaharakati nchini Bahrain, wameandamana kuanzia siku ya jumapili kushinikiza Serikali ya nchi hiyo kumuachilia huru mmoja wa wanaharakati ambaye yupo kwenye mgomo wa kutokula. 

Uwanja wa Bahrain ambao utatumika kwa mbio za mwaka huu za langalanga
Uwanja wa Bahrain ambao utatumika kwa mbio za mwaka huu za langalanga Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati walioandaa maandamano hayo wamedai kuwa endapo Serikali haitomuachilia huru Abdulhadi al-Khawaja, maandamano yao yataendelea na kupinga kufanyika kwa mbizo za magari za langalanga.

Wanaharakati hao wanataka kujiuzulu kwa mtoto wa mfalme Khalifa bin Salman Al-Khalifa ambaye ni waziri wa mambo ya nje wakisema ndie aliyechangia kuendelea kushikiliwa kwa mwanaharakati huyo.

Hivi karibuni Serikali ya Bahrain ilitangaza kuwa tayari kuandaa mashindano ya mbio za magari ya langalanga baada ya kuahirishwa mwaka jana kufuatia maandamano kama hayo.

Maandamano haya mapya yameitishwa kuinga kufanyika kwa mbio hizo nchini humo wakati bado kuna watu wanaendelea kushikiliwa na Polisi bila ya kufunguliwa mshataka toka walipokamatwa mwaka jana.

Shrikisho la mchezo huo limesema mbio hizo zitafanyika kama zilivyopangwa kwakuwa tayari wamehakikishiwa usalama na Serikali ya Bahrai ingawa kuna dalili kuwa mbio hizo zilizopangwa kufanyika tarehe 22 ya mwezi huu zisifanyike kwa mara nyingine.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.