Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Arsenal yaangukia pua kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Wigan

Ligi kuu nchini Uingereza imeendelea siku ya jumatatu kwa kushuhudia mchezo mmoja pekee ukipigwa kwenye dimba la Emarates kati ya wenyeji Arsenal waliowakaribisha vijana wa Wigan Athletics.

Roberto Martinez kocha mkuu wa Wigan akifurahia ushindi wa timu yake
Roberto Martinez kocha mkuu wa Wigan akifurahia ushindi wa timu yake Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mchezo huo ambao ulikuwa muhimu kwa timu zote mbili, ambapo wakati Arsenal ilikuwa ikihitaji ushindi ili kuendelea kusalia kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, Wigan wenyewe walikuwa wakihitaji ushindi ili kujinasua kwenye wimbi la kutaka kushuka daraja.

Kwenye mchezo huo Wigan ndi waliokuwa wa kwanza kujiandikia bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wake Franco Di Santo ambaye alipachika bao hilo katika dakika ya 7 ya mchezo.

Kabla Arsenal hawajajipanga kurejesha bao, walijikuta wakiruhusu bao la pili kwenye dakika ya 8 ya mchezo bao ambalo lilifungwa na Jordi Gomez aliyetumia uzembe wa mlinda mlango wa Arsenal na kuiandikia bao la pili timu yake.

Arsenal walizidisha mashambulizi  kwenye kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 27 ya mchezo lililofungwa na Thomas Vermaelen aliyeunganisha mpira wa kichwa.

Kwa matokeo hayo Arsenal imeendelea kusalia kwenye nafasi yake ya nne kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 64, wakati Wigan wamechumpa hadi kwenye nafasi ya kumi na sita wakiwa na alama 34.

Msimamo wa ligi unawaonyesha Manchester United wakiongoza ligi wakiwa na alama 82 wakati Manchester City wakiwa na alama 77, huku mkiani mwa ligi hiyo kukiwa na timu ya Wolves, Blackburn na Bolton.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.