Pata taarifa kuu
BAHRAIN

Mafundi wa kampuni ya Force India washambuliwa nchini Bahrain siku 2 kabla ya kufanyika kwa mbio za magari ya Langalanga

Wakati ikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kufanyika kwa mashindano ya langalanga nchini Bahrain, mashindano hayo yapo kwenye hatihati ya kutofanyika kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo. 

Madereva Michael Schumacher na Mark Webber wakiwa kwenye mbio za mwaka 201o nchini Bahrain
Madereva Michael Schumacher na Mark Webber wakiwa kwenye mbio za mwaka 201o nchini Bahrain Reuters
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zilizopatikana nchini humo hii leo zimesema kuwa gari lililokuwa limewabeba mafundi wa kampuni ya force India limeshambuliwa kwa roketi ingawa hakuna mtu ambaye amejeruhiwa kwenye shambulio hilo.

Wanaharakati nchini humo wamepanga kuendelea na maandamano yao licha ya serikali kutapiga marufuku wakishinikiza kuachiliwa kwa wanaharakati ambao wanashikiliwa na polisi bila ya mashtaka kwa muda mrefu.

Madereva mbalimbali wameanza kuwasili nchini humo huku wengi wao licha ya maandamano yanayoendelea wameoneshwa kuridhishwa na maandalizi ya nchi hiyo na kuonesha matumaini yao ya kufanyika kwa mashindano ya mwaka huu.

Dereva Mark Webber wa kampuni ya Red Bull alinukuliwa hapo jana akipongeza uamuzi wa chama cha mchezo huo kusisitiza kuwa mashindano ya mwaka huu ya nchini Bahrain yatafanyika kama yalivyopangwa licha ya maandamano ambayo yameendela nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.