Pata taarifa kuu
BAHRAIN GRAND PRIX

Lewis Hamilton aongoza kwenye mazoezi ya awali kuelekea mashindano ya Bahrain Grand Prix

Hatimaye madereva wa magari ya langalanga wameanza mazoezi yao hii leo nchini Bahrain licha ya maandamano yanayofanyika nchini humo kupinga mashindano hayo.

Dereva wa kampuni ya MacLaren, Lewis Hamilton
Dereva wa kampuni ya MacLaren, Lewis Hamilton Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hapo jana mafundi wa kampuni ya Force India walishambuliwa kwa kitu chenye mlipuko lakini walifanikiwa kutoka salama kwenye ajali hiyo na leo walishiriki mazoezi ya awali ya michuano ya Bahrai Grand Prix.

Mpaka sasa madereva wanaoongoza kwenye mazoezi ya awali ni Nicolas Rosberg wa kampuni ya Mercedes, akifuatiwa na Mark Webber wa kampuni ya Redbull, na nafasi ya tatu ikishikiliwa na Sebastian Vettel wa kampuni ya Redbul.

Nafasi ya nne inashikiliwa na Michael Schumacher wa kampuni ya Mercedes, nafasi ya tano inashikwa na Kobayashi wa kampuni ya Sauber na nafasi ya sita inashikiliwa na Fernando Alonso wa kampuni ya Ferrari.

Katika hatua nyingine kampuni ya Force India imetangaza kuwa haitoshiriki mazoezi ya pili kutokana na sababu ambazo hawajaziweka wazi.

Katika hatua nyingine, polisi nchini humo hapo jana na hii leo wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya maelfu ya waandamanji ambao walijitokeza kwenye mji wa Manama kupinga mashindano hayo kufanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.