Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Goli la Wayne Rooney lashinda Tuzo ya Goli Bora katika misimu 20 ya Ligi Kuu Nchini Uingereza

Goli la Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uingereza anayekipiga katika Klabu ya Manchester United Wayne Rooney limeshinda na kuwa goli bora katika kipindi cha misimu 20 tangu Ligi Kuu Nchini Uingereza ibadilushwe jina.

Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney akifunga goli dhidi ya Manchester City lililochaguliwa kuwa goli bora katika misimu 20 ya Ligi Kuu Uingereza
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney akifunga goli dhidi ya Manchester City lililochaguliwa kuwa goli bora katika misimu 20 ya Ligi Kuu Uingereza
Matangazo ya kibiashara

Goli la Rooney lililofanikiwa kushinda tuzo hiyo ni lile ambalo alilifunga katika mchezo dhidi ya Manchester City msimu uliopita ambapo alipiga tikitaka kuunganisha mpira uliopigwa na Luis Nani.

Goli la Rooney limeshinda baada ya kupata asimili 26 ya kura ambazo zilipigwa na kufutiawa na goli alilolifunga Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkamp katika mchezo dhidi ya Newcastle mwaka 2002.

Nafasi ya tatu kwa goli bora katika kuadhimisha miaka 20 ya Ligi Kuu Nchini Uingereza imekamatwa na Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry akifunga kwenye mchezo dhidi ya Manchester United.

Rooney baada ya goli lake kuchaguliwa kuwa bora katika misimu 20 ya Ligi Kuu hakusita kueleza namna ambavyo alivyofurahishwa na kuweka bayana kuna magoli ya wachezaji wengi ambayo yalikuwa yanamvutia tangu akiwa mtoto.

Rooney amesema magoli kama ya kina Alan Shearer, Paolo Di Canio, Tony Yeboah na David Beckham yalikuwa bora zaidi lakini kupata nafasi ya kushindanishwa nayo na kisha kuibuka mshindi ni heshima kubwa kwake.

Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Uingereza amewashukuru mashabiki wake wote kutokana na kumchagua kushinda tuzo hiyo wakati huu ambapo wakiadhimisha miaka 20 baada ya kubadilishwa kwa jina na kuitwa Ligi Kuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.