Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Robin Van Persie akataa kuongeza mkataba mpya na Klabu yake ya Arsenal

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uholanzi anayekipiga katika Klabu ya Arsenal Robin van Persie ametangaza hatokuwa tayari kusaini mkataba mpya na klabu yake ya sasa kutokana na kushindwa kuafikiana baadhi ya mambo ya Uongozi wa klabu hiyo.

Nahodha na Mshambuliaji wa Arsenal Robin Van Persie ambaye amekataa kuongeza mkataba na Klabu yake
Nahodha na Mshambuliaji wa Arsenal Robin Van Persie ambaye amekataa kuongeza mkataba na Klabu yake
Matangazo ya kibiashara

Van Persie ametangaza kutokuwa tayari kusaini mkataba mpya na Arsenal kutokana na mazungumzo baina yake, kocha Mkuu Arsene Wenger na Mkurugenzi mtendaji Ivan Gazidis kushinda kukubaliana kwenye masuala muhimu.

Mfungaji Bora huyo wa ligi Kuu nchini Uingereza amesema pande hizo tatu zimeshindwa kuafikiana katika kuhakikisha nchi hiyo inasonga mbele ikiwa ni pamoja na mapendekezo yake kupuuzwa.

Nahodha huyo wa Arsenal kutokana na uamuzi wake amebakiwa na miezi kumi na miwili tu kuichezea klabu hiyo kabla ya kuwa mchezaji huru wakati huu ambapo klabu kadhaa Barani Ulaya zikimezea mate saini yake.

Van Persie amesema ametafakari kwa muda mrefu sana juu ya hatima ya Arsenal na alipoona hakuna mustakabali mwema ameona ni vyema asiongeze mkataba wa kuendelea kuwepo Emirates.

Licha ya Van Persie ambaye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Nchini Uingereza msimu uliopita ataamua kuondoka mapema Emirates kabla ya mkataba wake haujaisha aua ataendelea kuitimika kwa shingo upande kwa muda ambao umesalia.

Klabu ya Arsenal yenyewe imejibu kauli ya Van Persie ya kukataa kuongeza mkataba kwa kusema wanaheshimu uamuzi wake na mchango wake ambao ameutoa kwa kipindi chote ambacho amekuwepo Emirates.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.