Patrice Muamba astaafu kucheza soka
Fabrice Muamba mchezaji wa soka katika klabu ya Bolton Wanderers nchini Uingereza ametangaza kustaafu kucheza soka.
Imechapishwa:
Tangazo lililotolewa katika mtandao wa klabu hiyo, limesema Muamba mwenye umri wa miaka 24 amechukua uamuzi huo kutokana na sababu za kiafya.
Muamba alizirai wakati akiichezea klabu yake ya Bolton dhidi ya ya Tottenham Hotspurs katika taji la kutafuta ubingwa wa kombe la FA na moyo wake kusimama kwa dakika 78.
Kupona kwa Muamba mzaliwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuliwashangaza wengi huku wakijiuliza ikiwa ataendelea tena kucheza soka.
Muamba ambaye pia aliwahi kuichezea Arsenal na Birmingham City amesema amefurahi na kuridhishwa hadi pale alikocheza soka na kuwashukuru mashabiki waliokuwa naye wakati mgumu akipata matibabu na kucheza soka nchini Uingereza.