Pata taarifa kuu
SOKA

Van Persie kuichezea Manchester United kujulikana

Vlabu vya soka vya Uingereza Manchester United na Arsenal, vimekuwa katika mazungumzo ya mwisho mwisho kuhusu usajili  wa mshambulizi wa Arsenal Robin van Persie.

Matangazo ya kibiashara

Arsenal imesema kuwa itamuuza Van Persie kwa kima cha Pauni Milioni 20 katika usajali unaofanyika siku chache kabla ya kuanza kwa msimu wa soka wa mwaka 2012/2013 siku ya Jumamosi.

Van Persie atakumbukwa sana katika klabu ya Arsenal baada ya kuifungia klabu hiyo mabao 37 msimu uliopita.

Manchseter United imeonesha nia ya kumsajili Van Persie huku Manschester City ikisema kuwa atakuwa na nafasi kubwa ikiwa atachezea klabu yao.

Wachambuzi wa soka nchini Uingereza wanaona kuwa ni bora Arsenal imuuze Van Persie ambaye tayari amesema kuwa hataki kuichezea tena Arsenal  na hataongeza mkataba wake na klabu  hiyo.

Van Persie amesema kuwa anataka kuichezea Manchester United au Juventus ya Italia huku mchezaji mwingine Alex Song akionesha nia ya kukihama klabu hiyo na kwenda kuicheza Barcelona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.