Pata taarifa kuu
SOKA

Van Persie akaribishwa Old Trafford

Hatimaye Robin Van  Persie amejiunga rasmi na klabu ya soka ya Uingereza ya Manchester United, na kusema kuwa imekuwa fahari kusajiliwa na klabu  hiyo ambayo  ataichezea kwa kipindi cha miaka minne ijayo.  

Matangazo ya kibiashara

Kwingineko, kocha wa klabu ya soka ya Arsernal nchini Uingereza Arsene Wenger, amesema huenda akampoteza kiungo wake wa kati Alex Song baada ya Robin Van Persie kuhamia Manchester United.

Wenger ameongeza kuwa  licha ya kutokuwepo kwa klabu inayomtaka Song kwa sasa, kumekuwa na uvumi kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon  huenda akahamia Barcelona nchini Uhispania.

Van Persie aliyeifunguia Arsenal mabao 37 msimu uliopita anatambulishwa Ijumaa kwa wachezaji na mashambiki wa Manchester United katika uwanja wa Old Trafford.

Klabu ya Arsenal ilikubali kuumuuza mchezaji huyo wa kimatifa kutoka Uholanzi kwa kima cha Pauni Milioni 24 baada ya maafikiano na Manchester United.

Manchseter United ilionesha nia ya kumsajili Van Persie baada ya mchezaji huyo kusema kuwa anataka kuichezea klabu hiyo na hataki tena kuichezea Arsenal msimu huu.

Wachambuzi wa soka nchini Uingereza wanaona kuwa imekuwa busara kwa Arsenal kumuuza Van Persie badala ya kumwacha kuondoka katika klabu hiyo mwenyewe.

Van Persie alijiunga na Arsenal akiwa na miaka 20 mwaka 2004 na kujiunga kwake katika klabu ya Manchester United kumeelezwa pia na wachambuzi wa soka kuwa kutasaiadia Manchester United kunyakua taji hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.