Pata taarifa kuu
UHISPANIA

Mourinho achukizwa na mlolongo wa matokeo mabaya ya Real Madrid kwenye La Liga msimu huu

Kocha Mkuu wa Real Madrid Jose Mourinho amechukizwa na mwenenendo mbaya wa Timu yake kwenye Ligii nchini Uhispania mwaka huu kutokana na kuwa na matoke mabaya yakichangiwa na kufungwa na Sevilla.

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho akiwa anafuatilia mchezo kwa makini lakini amekiri kuchukizwa na mwenendo wa Klabu yake
Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho akiwa anafuatilia mchezo kwa makini lakini amekiri kuchukizwa na mwenendo wa Klabu yake © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mourinho amehoji uwezo na morali ya wachezaji wake kutokana na kucheza michezo minne ya ligi na kuambulia pointi nne pekee kitu ambacho kimeanza kuzua maswali kama Real Madrid itaweza kutetea ubingwa wake.

Mourinho ameonekana kutokuwa na raha kabisa baada ya kushuhudia wakipoteza michezo miwili kwenye ligi ya msimu huu wakati mahasimu wao Barcelona wakiendelea kuchanja mbunga kwa kushinda michezo yao yote minne.

Kocha huyo mwenye maneno mengi na anatambulika kwa jina la Special One amekitaka kikosi chake kubadilika na kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wa kwanza wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Manchester City.

Mourinho amewaambia wanahabari timu yake haichezi vizuri kabisa kitu ambacho kinampa wasiwasi ya kwamba msimu huu hana kikosi imara cha kupambana na kushinda mataji licha ya kuanza kwa kushinda Super Cup.

Kocha huyo Mreno ameongeza kama timu haina wachezaji ambao wanajitolea inakuwa vigumu kuweza kupata ushindi na kutimiza malengo ya kutwaa mataji mengi kama ambavyo wengi wamekuwa wakifikiri.

Mourinho hakuacha kuisifia Sevilla kwa ushindi ambao wameupata na kuweka bayana bila ya wasiwasi yoyote walistahili kushinda kutokana na kuonesha mchezo mzuri dhidi ya Real Madrid.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea amekataa kata kata kushusha lawama zake kwa Cristiano Ronaldo akiamini kile ambacho kimetokea ni suala la kawaida kwa mchezaji yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.