Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Arsenal yapata ushindi dhidi ya Reading na kutinga Robo Fainali ya Kombe la Ligi

Klabu ya Arsenal ilifanikiwa kutoka nyuma kwa magoli manne kwa bila na hatimaye kupata ushindi wa magoli 7-5 katika mchezo wa Komba la Ligi dhidi ya Reading na hivyo kutinga katika hatua ya Robo Fainali. Mchezo huo uliopigwa katika Dimba la Madejski ulishuhudia Arsenal ikienda kupumzika ikiwa nyuma kwa magomi 4-1 kitu ambacho kilionesha timu hiyo huenda ingepoteza mchezo huo muhimu kwao.

Wachezaji wa Arsenal Theo Walcott na Olivier Giroud wakishangilia moja ya goli walilofunga kwenye mchezo dhidi ya Reading
Wachezaji wa Arsenal Theo Walcott na Olivier Giroud wakishangilia moja ya goli walilofunga kwenye mchezo dhidi ya Reading
Matangazo ya kibiashara

Theo Walcott ndiye alikuwa shujaa kwa upande wa Arsenal baada ya kufanikiwa kufunga magoli matatu huku Marouane Chamakh akifunga magoli mawili na mengine mawili yakiweka kimiani na Laurent Koscielny na Olivier Giroud.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri walitoka kwenye janga na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa kipekee na hiyo ilichangiwa kwa kiwango kikubwa na washabiki ambao wameendelea kuwaunga mkono.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Reading Brian McDermott amekiri hayo ni mauaji makubwa ambayo yalitokea katika kipindi cha pili na hivyo kwa sasa wanajipanga kwa ajili ya michezo yao ya Ligi.

Matokeo mengine yameshuhudia Leeds United ikaibuka na ushindi wa magoli 3-0 mbele ya Southampton na kufanikiwa kuingia Robo Fainali huku Middlesbrough ikavuna ushindi mwembamba wa goli moja kwa nunge mbele ya Sunderland.

Aston Villa ikafanikiwa kupata ushindi wake wa ugenini wa magoli 3-2 mbele ya Swindon Town wakati Bradford City wakipata ushindi kwa njia ya matuta kwa kuwafunga Wigan Athletic kwa penalti 4-2.

Michezo ya Kombe la Ligi inatarajiwa kuendelea hii leo ambapo Chelsea watakutana na manchester United wakati Norwich wakiwa nyumbani watakuwa na kibarua mbele ya Tottenham huku shughuli nyingine ikiwa ni kati ya Liverpool dhidi ya Swansea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.