Pata taarifa kuu
SOKA

Arsenal yaandikisha matokeo mabaya, Sunderland ni afueni

Kocha wa klabu ya soka ya Uingereza Arsenal, Arsene Wenger amekataa kuwatuhumu wachezaji wake baada ya klabu hiyo kufungwa na klabu ya daraja la pili Bradford FC mabao 3 kwa 2 kupitia mikwaju ya penalti wakati wa mchuano wa robo fainali ya kuwania taji la League Cup .

Matangazo ya kibiashara

Arsenal ilikuwa na matumaini ya kushinda mchuano huo katika muda wa ziada lakini bahati haikusimama licha ya Thomas Vermaelen kulazimisha sare katika dakika 88 ya mchuano huo.

Arsenal ambayo ni ya saba kwa alama 24 katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza na imekuwa ikishtumiwa kwa kutofanya vizuri katika ligi kuu ya soka msimu huu tangu kuondoka kwa mchezaji wake wa zamani Robin Van Persie ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Manchester United.

Katika hatua nyingine, klabu ya Sunderland imeondoka katika orodha ya timu zinazotarajiwa kushuka daraja katika ligi kuu ya Uingereza baada ya kuishinda Reading mabao 3 kwa 0.

Ushindi huo umewafikisha hadi katika nafasi ya 15 kwa alama 16 huku Reading ikiwa katika nafasi ya 19 kwa alama tisa.

Kocha wa Sunderland Martin O'Neill amesema ushindi huo umempa afueni na sasa ana matumaini ya kusalia katika ligi Kuu ya Uingereza msimu ujao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.