Pata taarifa kuu
Thailand

Viongozi wa Soka kutoka Bahrain na Thailand wajitokeza kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka barani Asia

Viongozi wa vyama vya soka kutoka nchini Thailand na Bahrain wamejotokeza kuwania ungozi wa soka katika shirikisho la soka barani Asia kuchukua nafasi ya Mohammed Bin Hammam aliyeondolea na shirikisho la soka duniani FIFA kwa tuhuma za kuhusika na ufisadi mwaka uliopita.

Mohammed bin Hamman aliyefungiwa na FIFA kushiriki katika shughuli za Mchezo wa Soka
Mohammed bin Hamman aliyefungiwa na FIFA kushiriki katika shughuli za Mchezo wa Soka
Matangazo ya kibiashara

Wagombea hao ni pamoja na Worawi Makudi kutoka Tahailand na Sheikh Salman bin Ibrahim al-Khalifa wa Bahrain.

Uchaguzi wa shirikisho hilo utafanyika mwezi wa Mei mwaka huu.

Kwa sasa shirikisho hilo linaongozwa na Zhang Jilong ambaye anashikilia uongozi huo kwa muda na pia anapewa nafasi kubwa kushinda katika uchaguzi huo.

Bin Hammam mwenye umri wa miaka 63 alikuwa akishutumiwa kufanya jaribio la kununua kura katika uchaguzi wa kumpata Rais wa FIFA uliofanyika Mwaka 2011, ambapo alikuwa akipambana na Sepp Blatter hivyo alifungiwa kujishirikisha na Mchezo wa Soka.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.