Pata taarifa kuu
ATP WORLD TOUR

Novak Djokovic afanikiwa kutetea taji lake la dunia dhidi ya Rafael Nadal

Mchezaji Tenesi nambari mbili kwa ubora wa mchezo huo duniani Novak Djokovic hatimaye amefanikiwa kutetea taji lake la dunia la mchezo huo baada ya kumfunga Rafael Nadal kwenye mchezo wa fainali. 

Novak Djokovic akiangalia kikombe ambacho amekitwaa hiyo jana baada ya kumshinda Rafael Nadal
Novak Djokovic akiangalia kikombe ambacho amekitwaa hiyo jana baada ya kumshinda Rafael Nadal Reuters
Matangazo ya kibiashara

Djokovic ambaye alipoteza nafasi yake ya kwanza kwa rafael Nadal mwezi mmoja uliopita, hapo jana alikuwa mwiba kwa mpinzani wake na kufanikiwa kumdhibiti kwa muda wote wa mchezo.

Djokovic ambaye ni raia wa Serbia, amefanikiwa kutetea taji lake kwa kumfunga Nadal kwa seti mbili mfululizo kwa matokeo ya 6-3 na 6-4 kwenye mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa O2 jijini London.

Kufuatia ushindi huo Nadal amefanikiwa kuongeza historia kwenye kitabu chake cha kumbukumbu baada ya hapo jana kufikisha mechi ya ishirini na mbili mfululizo bila kupoteza akimaliza msimu wake wa mwaka 2013 kwa mafanikio katika miaka mitatu mfululizo.

Djokovic hivi sasa ameelekea mjini Belgrade, Jamhuri ya Czech ambapo siku ya Ijumaa atashiriki fainali za michuano ya Davis.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Djokovic anasema amefurahishwa na kiwango alichonacho kwasasa na pia kumpongeza mpinzani wake kwa kuonesha mchezo mzuri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.