Pata taarifa kuu
Michezo

Southampton kukutana na Arsenal Ugenini

Southampton ambao wameonyesha ukali watakumbana na kibarua chao kigumu zaidi katika Ligi ya Premia msimu huu Jumamosi watakapokutana na Arsenal ugenini.

Arsenal itaumana na Southampton mwishoni mwa juma hili
Arsenal itaumana na Southampton mwishoni mwa juma hili telegraph.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, hilo halimbabaishi hata kidogo meneja Mauricio Pochettino, na wala haliwatishi washambuliaji wake matata Rickie Lambert na Jay Rodriguez.

Saints wamo nambari tatu kwenye ligi baada ya kucheza mechi 11, wakiwa na alama 22 ambazo ni tatu tu chini ya zile walizo nazo Arsenal ambao wanaongoza ligi.

Lakini Pochettino anaamini kwamba Saints wanaweza kuwalima viongozi hao wa ligi sawa na walivyowafanyia Liverpool walipokuwa wakiongoza ligi mapema kwenye msimu.

Raia huyo wa Argentina aliambia televisheni ya Southampton ya Saints Player kuwa anafikiri itakuwa mechi sawa na ya Liverpool kwa sababu walipokuwa wakicheza nao walikuwa juu kwenye ligi.

Mara zote wamekuwa wakijiamini kushinda kila mechi wanayocheza akisisitiza imani ambayo imeinua klabu hiyo ya kiwango cha kadiri kutoka pwani ya kusini hadi juu kwenye ligi kuu.

Pambano hilo linatokea baada ya muda wa mapumziko kwa ajili ya mechi za kimataifa ambapo wachezaji watatu wa Saints waliitwa kuchezea Uingereza kwenye mechi dhidi ya Chile na Ujerumani - Lambert, Rodriguez na nahodha Adam Lallana.

Pochettino alisema Waingereza hao watatu wako tayari kutamba kwenye klabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.