Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA

Kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere kutumikia adhabu ya mechi 2 za ligi: FA

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Arsenal inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza, Jack Wilshere ameadhibiwa na chama cha soka nchini humo kutocheza mechi mbili za ligi kutokana na kupatikana hatia ya kutoa ishara ya matusi kwenye mchezo wa timu yake Manchester City.

Jack Wilshere, kiungo wa Arsenal FC ya Uingereza
Jack Wilshere, kiungo wa Arsenal FC ya Uingereza Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wilshere mwenye umri wa miaka 21 hivi sasa amekiri mbele ya kamati maalumu iliyoundwa kumchunguza, lakini akapinga adhabu ya kutocheza mechi mbili kwenye timu yake.

Awali kinda huyu alikata rufaa kwenye kamati ya maadili ya chama cha soka nchini humo FA akitaka kutochukuliwa hatua kali, lakini madai yake yalitupiliwa mbali na kamati hiyo na kusisitiza mchezaji huyo kutumikia adhabu yake.

Picha za televisheni zilimuonesha Wilshere akionesha ishara ya kidole cha kati kwa mashabiki wa Manchester City waliokuwa wakishangilia ushindi wa magoli 6-3 dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wake wa nyumbani wa City of Manchester.

Kinda huyo ataanza kutumikia adhabu yake mapema iwezekanavyo ambapo hatoichezea timu yake kwenye mchezo muhimu wa ligi siku ya Jumatatu dhidi ya Chelsea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.