Pata taarifa kuu
SOKA-MICHUANO YA KLABU BINGWA UEFA

Michuano ya ligi ya UEFA yaingia mzunguko wa pili

Gareth Bale huenda akarejea katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid watakapomenyanna na Liverpool.

Gareth Bale mshambuliaji wa Real Madrid anatazamiwa kucheza mchuano wa leo Jumanne Novemba 4 dhidi ya Liverpool..
Gareth Bale mshambuliaji wa Real Madrid anatazamiwa kucheza mchuano wa leo Jumanne Novemba 4 dhidi ya Liverpool.. REUTERS/Sergio Perez
Matangazo ya kibiashara

Bale hajawahi kuichezea Real Madrid tangu tarehe 5 mwezi uliopita kutokana na jeraha.

Kocha Carlo Anceloti amesema hana uhakikia ikiwa mshambuliaji huyo atacheza leo Jumanne Novemba 4.

Kwa upande wa Liverpool, Daniel Sturridge huenda asicheze leo licha ya kwenda Madrid, amekuwa nje ya kikosi cha Liverpool kutokana na jeraha la paja.

Wachezaji wa Liverpool Steven Gerrard (kushoto) na Mamadou Sakho (kulia) katika uwanja wa Anfield, Aprili 27 mwaka 2014.
Wachezaji wa Liverpool Steven Gerrard (kushoto) na Mamadou Sakho (kulia) katika uwanja wa Anfield, Aprili 27 mwaka 2014. REUTERS/Darren Staples

Kocha Bredan Rodger amesema mechi ya leo ni muhimu sana, kabla ya kukutana na Chelsea mwishoni mwa juma kumenyana na katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Hayo yakijiri, Zenit St Petersburg ya Urusi inaingia uwanjani Jumanne wiki hii kumenyana na Bayer Liverkusen ya Ujerumani, Arsenal itakuwa nyumbani Emerates wakiwakaribisha Anderletch ya Ubelgiji huku Juventus ya Italia ikipepetana na Olympiakos ya Ugiriki.

Manchester City watakwaruzana na CSKA Moscow ya Urusi Alhamisi wiki hii, FC Bayen Munchen watakwaruzana na AS Roma. Wakati huohuo Ajax Amsterdam watapambana na FC Barcelona. Paris St Germain watacheza na Apoel Nicosia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.