Pata taarifa kuu
SOKA-CAF

Mechi upande wa wanawake zapigwa katika viwanja mbalimbali

Michuano ya marudiano na ya mwisho kwa timu za taifa za soka kwa upande wa wanawake kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika itakayofanyika nchini Cameroon baadaye mwaka huu zinachezwa leo Jumanne.

Mazoezi ya timu ya taifa ya kandanda ya wanawake "Tembo wanawake" Côte d’Ivoire.
Mazoezi ya timu ya taifa ya kandanda ya wanawake "Tembo wanawake" Côte d’Ivoire. Maureen Grisot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mataifa manane yatashiriki katika fainali hiyo itakayochezwa kati ya tarehe 19 Novemba hadi tarehe 3 mwezi Desemba katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo jijini Yaounde na Stade Municipal de Limbe mjini Limbe.

Tayari Cameroon ambao ni wenyeji wameshafuzu.

Mataifa mengine ambayo pia yamefuzu ni pamoja na mabingwa wa mwaka 2008 na 2012 Equitorial Guinea ambao wanashiriki kwa mara ya tano katika mashindano haya.

Misri ambayo inashiriki kwa mara ya pili nayo imeshafuzu pamoja na Zimbabwe ambayo haya ni makala yake ya nne kushiriki.

Mataifa manne yako mbioni kutafuta nafasi nne zinazosalia kucheza katika michuano hiyo ya kutafuta ubingwa wa Afrika.

Ratiba ya michuano ya leo Aprili 12, 2016

Kenya vs Algeria-Saa 9 mchana
Nigeria vs Senegal-Saa 12 jioni
Ghana vs Tunisia-Saa 12 Jioni
Afrika Kusini vs Botswana-Saa 2 usiku

Mchuano wa Harambee Starlets ya Kenya na Algeria unasubiriwa sana na mashabiki wa soka nchini humo kwa sababu ikiwa Kenya itashinda, itashiriki katika michuano hiyo ya Afrika kwa mara ya kwanza.

Mechi ya kwanza ugenini warembo hao kutoka Kenya walilazimisha sare ya mabao 2 kwa 2 jijini Algiers.

Mchuano huo utapigwa katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi na Shirikisho la soka nchini humo FKF limesema hakutakuwa na kiingilio ili mashabiki wafike kwa wingi kuishangilia timu yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.