Pata taarifa kuu
CAF-AFRIKA-SOKA

Nusu fainali ya klabu bingwa kuanza kupigwa Jumanne usiku

Michuano ya soka ya mzunguko wa kwanza, hatua ya nusu fainali kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, inachezwa siku ya Jumanne.

ES Tunis na Al-Ahly wakicheza katika mechi iliyopita
ES Tunis na Al-Ahly wakicheza katika mechi iliyopita STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Al-Ahly ya Misri itakuwa nyumbani jijini Cairo, kumenyana na ES Setif ya Algeria huku Primero de Agosto ya Angola ikiwakaribisha Esperance de Tunis ya Tunisia jijini Luanda.

Al-Ahly ambao wanashikilia rekodi ya kushinda mataji mengi katika mahindano haya, walifuzu katika hatua hii baada ya kuishinda Horoya ya Guinea katika hatua ya robo fainali.

Mabingwa hao wa Misri, wameshinda taji hili la CAF mara nane, mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2013.

ES Setif nayo ilifuzu baada ya kuwashinda mabingwa watetezi, Wydad Casablanca ya Morocco katika hatua ya robo fainali.

Klabu hii inakwenda katika mechi hii ikiwa na rekodi ya kushinda taji hili mara mbili mwaka 1988 na 2014.

Hata hivyo, Primero de Agosto ambayo iliiondoa TP Mazembe ya DRC, imeweka historia kwa kufuzu kwa mara ya kwanza katika hatua hii.

Wapinzani wake Esperance de Tunis, wana rekodi ya kufika katika hatua hii mara kadha na kuwahi kushinda taji hili mara mbili mwaka 1994 na 2011.

Mechi hizi zinachezwa nyumbani na ugenini na mshindi atafuzu kucheza fainali, itakayopigwa mwezi Novemba.

Mechi za nusu fainali kuwania taji la CAF, kupigwa

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.