Pata taarifa kuu

Simba, Vita Club na Mazembe katika mtihani mwingine CAF

Msikilizaji vinara wa kundi A katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika, klabu ya Simba ya Tanzania, Jumatatu hii inatupa karata yake nyingine kujaribu kuendelea kusalia kileleni mwa kundi lake ambapo itakuwa nyumbani nchini mwake kuwakaribisha Al Merreikh ya Sudan.

Kikosi cha wachzaji wa klabu ya Simba ya Tanzania
Kikosi cha wachzaji wa klabu ya Simba ya Tanzania © CafOnline Media
Matangazo ya kibiashara

Simba yenye alama 7 kibindoni kwenye kundi lake, inaingia uwanjani huku ikiwa na rekodi nzuri ya mechi zake za awali.

Katika mchezo wake wa kwanza majuma kadhaa nyumba, simba ilichomoza na ushindi dhidi ya mabingwa watetezi klabu ya Al Ahly ya Misri, kabla ya kushinda mchezo wake uliofuata dhidi ya Vita Club ya DRC na baadae kutoka sare na Al Merreikh ya Sudan, mchezo uliopigwa Khartoum.

Katika mchezo wa leo simba ina hitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano, na ikiwa itafanikiwa kushinda hivi leo, itakuwa timu ya kwanza kujihakikishia tiketi ya hatua ya mtoano wa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Hata hivyo tofauti na mechi zake za awali ambazo ilicheza nyumbani na kuruhusu mashabiki, safari hii timu hiyo haitakuwa na mashabiki uwanjani kufuatia uamuzi wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, kuaigiza klabu hiyo kutoruhusu mashabiki uwanjani.

CAF inasema Simba ilikiuka makataa ya kukabiliana na maambukizi ya Covid 19 ambapo mashabikik wake hawakuzingatia njia za kujikinga licha ya Serikali ya Tanzania kuwa haijakataza mashabiki uwanjani.

Uamuzi wa CAF umekosolewa vikali na mashabiki wa soka nchini Tanzania ambao wanaona ni njama za CAF kujaribu kuikosoesha Simba ushindi kwa kuwa mashabiki wamekuwa chachu kubwa ya ushindi wake nyumbani.

Katika mchezo mwingine wa kundi A, Al Ahly ya Misri watakuwa nchini DRC kucheza na Vita Club, katika mchezo muhimu kwa timu zote ukizingatia mara ya mwisho kukutana juma moja lililopita, zilitoshana nguvu ya magoli 2-2, timu zote mbili zikiwa na alama 4 sawa.

Timu nyingine ya DRC, TP Mazembe, ambayo ikok kundi B, itakuwa ugenini dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, inayomilikiwa na rais mpya wa shirikisho la soka Afrika CAF, Patrice Motsepe.

Mamelod inaongza kundi lake ikiwa na alama 9, ikifuatiwa na TP Mazembe yenye alama 2 sawa na Al Hilal Omdurman na Belouizdad.

Mechi zingine za hivi leo ni pamoja na Petro de Luanda itakayokuwa nyumbani kuwakaribisha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, hukuj Horoya ya Guinea, itakuwa inawakaribisha Wydad Casablanca ya Morocco, huku MC Algier ya Algeria itakuwa nyumbani dhidi ya Teungueth.

Mabingwa wa zamani klabu ya Zamalek yenyewe itakuwa nyumbani dhidi ya ES Tunis ya Tunisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.