Pata taarifa kuu

Wydad, Sundowns zatinga robo fainali, Simba yahitaji alama moja tu

Klabu ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu bingwa barani Afrika, baada ya kuchomoza na ushindi wa goli 1 kwa 0 dhidi ya TP Mazembe ya DRC.

Wachezaji wa klabu ya Al Ahly ya Misri, wakifanya dua kabla ya mechi yao na AS Vita ya DRC, katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika, CAF
Wachezaji wa klabu ya Al Ahly ya Misri, wakifanya dua kabla ya mechi yao na AS Vita ya DRC, katika mashindano ya klabu bingwa barani Afrika, CAF © CafOnline Media
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu umeifanya Mamelod Sundowns kufikisha alama 12 na kuongoza kundi lake B.

Ikiwa zimesalimia mechi mbili za kukamilisha hatua ya makundi, Sundowns inaongoza kwa alama 9 zaidi dhidi ya timu inayoshikilia nafasi ya pili Al Hilal ambaye alitoka bila kufungana na klabu ya CR Belouizdad.

Goli pekee la Sundowns lilifungwa na Lebohang Maboe.

Klabu ya TP Mazembe inasalia ya mwisho katika kundi lake na alama 2, ikizidiwa alama moja tu na AL Hilal na CRB ambazo zote zina alama 3, ambapo mechi mbili za mwisho zitakuwa muhimu kwa timu zote tatu.

Katika kundi jingine, Klabu ya Wydad Casablanca, yenyewe imejihakikishia zaidi nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu bingwa barani Afrika, licha ya kutofungana na Klabu ya Horoya ya Guinea.

Wydad imepoteza alama kwa mara ya kwanza katika hatua ya makundi, lakini inaongoza kundi lake kwa alama 10.

Nchini Tanzania, klabu ya Simba, maarufu kama "wekundu wa msimbazi", nao wamezidi kujikita kileleni mwa kundi lake ambapo sasa wanahitaji alama moja tu kufuzu hatua ya robo fainali ya klabu bingwa Afrika.

Simba imejihakikishia nafasi hiyo baada ya kupata ushindi mwingine wa mabao 3-0 dhidi ya El Merreikh ya Sudan, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa bila ya mashabiki kutokana na kuzuiwa na CAF.

Magoli mawili ya kipindi cha kwanza yaliyofungwa na Luis Miquissone na nahodha Mohammed Hussein na lile la tatu lililofungwa na Chris Mugalu, yalitosha kuipa alama tatu muhimu.

Hii imekuwa ni mechi ya 9 kwa Simba kutopoteza mchezo wowote katika uwanja wake wa nyumbani.

Hata hivyo mchezo huo uliingia dosari kidogo baada ya wachezaji takribani 8 wa El Merreikh, kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya Covid 19, vipimo ambavyo klabu hiyo ya Sudan ilisema inavipinga.

Kwa ushindi huu Simba imefikisha alama 10, alama tatu zaidi ya anayeshika nafasi ya pili klabu ya Al Ahly ambayo iliwafunga Vita Club ya DRC kwa mabao 3 mjini Kinshasa.

Al Ahly, wamefufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali baada ya ushindi dhidi ya SD Gita katika dimba la Stade des Martyrs.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.