Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA UINGEREZA- MSIMU MPYA

Maandalizi ya vilabu kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Uingereza

Baada ya miaka miwili ya kutatua na kabiliana na changamoto zilizosababishwa na janga la uviko 19, baadhi ya mechi zimeratibiwa kupigwa kama njia moja ya kunoa makali ya wachezaji kuelekea msimu mpya wa ligi kuu nchini Uingereza maarufu kama EPL.

Nembo ya ligi kuu nchini Uingereza
Nembo ya ligi kuu nchini Uingereza EPL
Matangazo ya kibiashara

Tayari baadhi ya timu kubwa zinazoshiriki katika ligi hiyo ya Uingereza yenye ufuasi mkubwa Afrika mashariki zinajiaanda kwa kushiriki mechi za kirafiki katika maeneo tofauti ya dunia.

Mechi hizo pia zinatumika kama njia moja ya kuwapa nafasi mashabiki wa vilabu hivyo walio katika nchi zengine duniani kukutana na wachezaji waowapenda kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa.

Baadhi ya wakufunzi wa timu hizi hutumia wakati huu wa mechi za kirafiki kupima nguvu vikosi vyao pamoja na mifumo tofauti ya uchezaji wanayoiamini.

Mechi hizi uenda zikasaidia timu au zikakosa.Manchester United wana mazoea ya kua na maandalizi bora ila wanaishia kukosa ubingwa.

Kocha wa As Roma Jose Mourinho aliwahi kuhojiwa kuhusu umuhimu wa maandalizi ya timu kabla ya msimu mpya na kusema kua hazina maana, lakini msimu uliofuata 2015-2016 akatimuliwa akiwa na chelsea ya Uingereza.

Baadhi ya makocha kama Pep Guardiola wa Manchester City na Jurgen Klopp wa Liverpool tayari wamewasajili wachezaji wenye majina makubwa katika viwanja vya mpira kama Darwin Nunez na Erling Haaland.

Baadhi ya mechi zimeratibiwa kupigwa kwa maandalizi ya msimu mpya

Leicester

Julai 31: Sevilla (Ugani King Power).

Liverpool

Julai 30: Manchester City (Ugani King Power)

J Julai 31: Strasbourg (Anfield)

Manchester United

Julai 30: Atletico Madrid (Uwanjani Ullevaal, Oslo)

Julai 31: Rayo Vallecano (Old Trafford)

Tottenham

Julai 30: Roma (Uwanjani Sammy Ofer, I-Tech Cup)

Arsenal imepata ya ushindi wa magoli 6 bila ya jibu dhidi ya Sevilla

Na Paul Nzioki

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.