Pata taarifa kuu

Michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika kwa vilabu inaendelea wikendi hii

NAIROBI – Michuano ya soka kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika inaendelea kupigwa mwishoni mwa wiki hii, zikiwa zimesalia mizunguko miwili, kutamatisha hatua ya makundi. 

Mashabiki wa  Wydad Casablanca
Mashabiki wa Wydad Casablanca AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Mshindi wa kwanza na wa pili, kutoka kila kundi, watafuzu katika hatua hiyo ya robo fainali. 

Mpaka sasa Raja Club Athletic ya Morocco ndio timu pekee inayocheza mechi ya tano wakiwa tayari wamefuzu kucheza hatua ya robo fainali.   

As vita club kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo watakua nyumbani wakiwakaribisha Wydad Casablanca, katika mchezo wa kundi A.   

Katika kundi hili, Wydad ya Morocco ndio viongozi wakiwa na alama 9, wao As Vita wakiwa wa mwisho. Mechi hii inapigwa saa Kumi Kamili Afrika Mashariki.   

Al Hilal Omdurman ya Sudan inayoongozwa na Kocha raia wa DRC Florent Ibenge watapambana na Mamelodi sundowns. Mechi hii itaamua kiongozi wa Kundi B lakini vilevile mshindi akipata nafasi ya kufuzu katika hatua ya robo fainali.    

Katika mechi ya mkondo wa Kwanza nchini Afrika kusini, Mamelodi Sundowns walishinda Al Hilal kwa goli moja bila ya jibu. Sundowns ni baadhi ya timu zinazonolewa na makocha wachanga.   

Wawakilishi wa Uganda, Vipers Sc watachuana na Raja Casablanca ya Morocco ambao tayari wamefuzu katika hatua ya robo fainali kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika.     

Nafasi ya Vipers ni finyu sana katika kundi hili wakiwa na alama moja pekee baada ya kucheza mechi nne.    

Katika mechi ya mwisho, timu hizi mbili zilipokutana, Vipers walipoteza kwa kufungwa magoli matano kwa sifuri.   

Simba sc kutoka Tanzania itaialika Horoya ya Guinea katika pambano la Kundi C litakalopigwa kuanzia saa Moja  usiku Afrika Mashariki ikihitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi katika robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika. 

Kocha wa timu hiyo, Roberto Oliveira 'Robertinho' amesema mastaa wa timu hiyo wameutazama mchezo huo kwa jicho la kipekee na wameapa kupambana kuwapa raha mashabiki na raia wa  Afrika Mashariki.   

Mechi ya mwisho leo ni Js Kablyie dhidi ya Petro Atletico ya Angola ambao watakua wanamtafuta mshindi wa pili kwenye kundi A.   

Na Paul Nzioki

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.