Pata taarifa kuu

KUSHINDWA KWA KLABU ZA DRC KATIKA MICHUANO YA CAF

NAIROBI – Na mchambuzi wetu Paul Nzioki

Nembo ya Shirikisho la soka nchini DRC
Nembo ya Shirikisho la soka nchini DRC FECOFA
Matangazo ya kibiashara

Imekua ni wiki ya michuano ya klabu bingwa barani afrika  na kombe la shirikisho, Ikichezwa katika hatua ya mwisho kwenye makundi. 

Timu nane tayari zimefuzu katika hatua ya robo fainali kwenye mashindano yote huku nane zikirudi nyumbani na Milioni 2.2 dola ya kimarekani kwa washiriki wa klabu bingwa na 275,000 dola ya Marekani kwa washiriki wa kombe la shirikisho. 

Tukio la mshangao ni kua hatuna timu hata moja kutoka Jamhuri ya kidemokrasia Congo iliyofuzu kuelekea robo fainali. 

Wawakilishi wa Drc katika pambano la klabu bingwa walikua ni As Vitaclub ambao wamemaliza katika nafasi ya mwisho katika Kundi A, Kundi waliojumuishwa pamoja na Kabylie ya Algeria na Petro Atletico kutoka Angola. 

Wachezaji wa  Wydad ya Morocco dhidi ya AS Vita Club  ya nchini DRC
Wachezaji wa Wydad ya Morocco dhidi ya AS Vita Club ya nchini DRC © Courtesy of CAF

Hii ni As Vita club iliyofika fainali ya klabu bingwa mwaka 2014 na kufanya hivyo tena mwaka 2018 kwenye kombe la shirikisho chini ya kocha  Jean-Florent Ikwange Ibengé. 

Kwenye kombe la shirikisho, walikuwepo Tp Mazembe, St Eloi Lupopo na DC Motema Pembe ambao wote wamerudi nyumbani. 

Mazembe ambao ni baadhi ya klabu zenye mafanikio makubwa kisoka katika jumuiya ya afrika mashariki wameshindwa hata katika mechi ya mwisho ikiwa na maana kwamba Yanga kutoka Tanzania iliwashinda nyumbani na ugenini. 

Kwa ajili ya kumbukumbu Mazembe mwaka 2015 ndio mara ya mwisho kushinda ubingwa wa afrika kwa vilabu vya soka kwa wanaume na mwaka 2010 walimaliza katika nafasi ya pili kwenye kombe la Dunia La FIFA Kwa vilabu. 

Moïse Katumbi Mmiliki wa TP Mazembe ya nchini DRC na mgombea wa urais
Moïse Katumbi Mmiliki wa TP Mazembe ya nchini DRC na mgombea wa urais AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

St. Eloi Lupoo walimaliza katika nafasi ya tatu kundi A nyuma ya Us Algers na Marumo Gallants na mbele ya Al Akhdar ya Libya. 

Dc Motema Pembe wamemaliza kinyonge katika kundi B nyuma ya Diables Noirs ya Congo, Rivers United ya Nigeria na Wa Ivory coast ASEC Mimosas. 

Hii ni aibu kwa washirika wanne kukosa mmoja wa kupeperusha bendera ya taifa na kuongeza idadi ya timu kutoka jumuiya hii kwenye jukwaa hili kubwa. Sasa macho yote ni kwa vilabu vya Tanzania  mapacha wa Kariokoo Simba na Yanga. 

Nini Kimechangia kushuka Viwango kwa timu Hizi 

Soka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kama ilivyo katika sehemu kubwa ya dunia inaingiliana na siasa. 

Katika nchi hiyo ya Afrika ya kati, vilabu vya soka kwa muda mrefu vimekuwa njia ya utawala ulio madarakani kujenga mtaji wa kisiasa. Wanasiasa wengi hujihusisha na vilabu ili kuimarisha taswira yao. Kwa upande mwingine, soka pia ni nafasi ya upinzani wa kisiasa. 

Wakosoaji wengi wa Serikali ya Rais Felix Tshekedi wanaamini Mazembe inayoongozwa na Moise Katumbi na aliye na nia ya kuwania Urais, haikupata uungwaji mkono kutoka kwa serikali. 

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi wakati akilihutubia taifa Ijumaa Oktoba 22 2021.
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi wakati akilihutubia taifa Ijumaa Oktoba 22 2021. © Ikulu ya Kinshasa DRC

Inaaminika Mazembe ndio timu yenye bajeti kubwa nchini DRC, ilhali hawakupata fedha kutoka kwa serikali ikiwalazimu kugharamikia maslahi yao kutoka mifukoni mwao. 

Wala bosi wa klabu ya Mazembe amenukuliwa akisema kando na hayo hatolalamika kuhusu fedha kama tatizo. 

Sababu ya pili, Mbele ya waandishi wa habari Machi 28 mjini Lubumbashi, rais wa TP Mazembe, Moïse Katumbi, kwa upande wake amelaumu Wizara ya Michezo. 

Kwa mujibu wa Tajiri Katumbi  kukosekana kwa michuano ya kitaifa kumesambaratisha juhudi za timu yake kufuzu katika hatua ya Robo. 

"Tulijipanga, lakini tuliondolewa. Na nadhani tunapaswa kushambulia shida halisi. Wachezaji hawana muda wa kucheza, hakuna automatisering, hatuwezi kutafuta tatizo kwingine, tatizo ni mpangilio wa michuano yetu. Je, ni matokeo gani tunayotarajia kwa timu zote za Kongo zinazocheza na vilabu vinavyocheza katika Ligi zao, ubingwa haupo tena nchini kwetu”, alisema Katumbi.

Michuano ya LINAFOOT  katika ligi ya 1 na 2 haiendelei kwa sasa baada ya kusitishwa  mapema mwakani kutokana na ukosefu wa viwanja vinavyokidhi mahitaji ya Mchezo wa soka na ugumu wa timu kusafiri katika mechi za Ugenini. 

Kufikia sasa bado Rais wa shirikisho la soka DRC (FECOFA) Donatien Tshimanga, Wizara ya Michezo na mkuu wa tume inayosimamia shughuli za Ligi, Dieudonne Sambi, wanaendelea kutafuta suluhu. 

Sababu ya tatu ni swala la Viwanja. Timu zote isipokua Mazembe walilazimka kucheza mechi zao nje ya taifa Lao kwa sababu uwanja pekee ulioidhinishwa na shirikisho la soka barani Afrika CAF ni uwanja wa Lubumbashi ambo unamilikiwa na Mazembe. 

Rais wa CAF  Patrice Motsepe
Rais wa CAF Patrice Motsepe AP - Themba Hadebe

Baadhi ya timu zilitoa madai kwamba haziwezi kutumia uwanja wa mpinzani wao. Hatua hii imezilazimu timmu hizi kucheza bila mashabiki ambao katika shabiki ni mchezaji wa kumi na mbili. 

La mwisho timu kama Mazembe ilifanya vizuri miaka ya zamani kwa sababu ya kuwajumuisha wachezaji wa kigeni jambo ambalo kwa sasa sio mbinu yao. Mazembe haina wachezaji wengi wa kigeni kama zamani. 

Tarehe 31 mwezi machi Mwanahabari wa michezo François Claude Kabulo Mwana Kabulo alipewa wadhifa wa Waziri wa Michezo wa DRC rasmi. 

Baadhi ya sababu zilizosababisha matokeo duni kwa vilabu hivi zinamsubiri kuzitatua. Changamoto hizo zinampata Mwana Kabulo pamoja na kuhakikisha Michezo ya 9 ya La Francophonie inafanikiwa na timu ya taifa Leopards inafuzu kwa michuano ya kombe la bara Afrika mwaka 2023. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.