Pata taarifa kuu

Tp Mazembe yamwajiri kocha wa zamani Lamine Ndiaye

NAIROBI – Uchambuzi wa Paul Nzioki.

Moïse Katumbi, Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe
Moïse Katumbi, Mmiliki wa klabu ya TP Mazembe AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Aliyekua Kocha wa Tp Mazembe, Lamine Ndiaye ametia saini mkataba wa kuinoa tena klabu hio ya Jamhuri ya kidemokrasia Congo kama kocha mkuu. 

Kulingana na taarifa iliyochapishwa na kituo cha Radio Okapi, rais wa klabu hiyo Moïse Katumbi, amefufua imani yake kwa Ndiaye, baada ya kushindwa katika Kombe la Shirikisho la CAF, la mwaka huu wa 2023. 

Taarifa kutoka kwa wandani wake pia zinaarifu kua, Ndiaye raia wa senegal amepewa misheni ya kujiandaa vyema kwa michuano ijayo, ikiwa ni pamoja na Super League, na uwezekano wa kuanza tena kwa Ligi ya kandanda DRC (LINAFOOT). 

Moïse Katumbi Mmiliki wa TP Mazembe ya nchini DRC na mgombea wa urais
Moïse Katumbi Mmiliki wa TP Mazembe ya nchini DRC na mgombea wa urais AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Kwa mujibu wa mchambuzi wa Gazeti maarufu nchini Tanzania Mwanaspoti, mjini Lubumbashi, DR Congo, Iragi Elisha muda wowote, TP Mazembe itamtambulisha rasmi Kocha huyo. 

Chini ya N'Diaye, Mazembe iliwahi kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia. Pia ilitwaa taji moja la Ligi ya Mabingwa Afrika lakini pia mataji mawili ya Caf Super Cup. 

N'Diaye aliipa TP Mazembe mataji matatu ya Ligi Kuu ya DR Congo na anatajwa kama miongoni mwa makocha bora wa Kiafrika kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata katika taaluma hiyo. 

Mbali na TP Mazembe, N'Diaye amewahi kuwa kocha wa Coton Sport ya Cameroon kuanzia 2003 hadi 2006 na baadaye kuwa kocha wa timu ya taifa ya Senegal mnamo Januari 2008, kufuatia kujiuzulu kwa Henryk Kasperczak ambaye  alifutwa kazi kama meneja Oktoba 2008. 

Sadio Mané wa Senegal wakati wa mechi za CHAN mwaka huu
Sadio Mané wa Senegal wakati wa mechi za CHAN mwaka huu AFP - JOHN WESSELS

Ndiaye aliteuliwa kuwa meneja wa timu ya Morocco ya Maghreb Fez mnamo Desemba 2008 ambayo aliitumikia hadi 2010 alipotimkia TP Mazembe. 

Mnamo Desemba 2014 alikua mkurugenzi wa ufundi wa AC Léopards. Kufikia Julai 2018 alikuwa meneja wa klabu ya Al-Hilal ya Sudan na Novemba 2019 alikua meneja wa klabu ya Guinea ya Horoya AC. 

Taarifa ya TP Mazembe imeeleza kuwa urejeo wa N'Diaye unalenga kuirudisha timu hiyo katika makali yake ya zamani ambayo kwa sasa yanaonekana kupotea. 

Mazembe wameondolewa katika mashindano ya kombe la shirikisho barani Afrika, wakipoteza mechi ya mwisho katika hatua ya makundi dhidi ya Young Africans ya Tanzania. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.