Pata taarifa kuu

UEFA kusaidia soka la wanawake Uganda.

NAIROBI – Na Paul Nzioki

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA linatoa mafunzo kwa siku nne, kukuza uwezo wa uongozi wa mchezo huo nchini Uganda.
Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA linatoa mafunzo kwa siku nne, kukuza uwezo wa uongozi wa mchezo huo nchini Uganda. REUTERS - DENIS BALIBOUSE
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA linatoa mafunzo kwa siku nne, kukuza uwezo wa uongozi wa mchezo huo nchini Uganda.

Warsha hiyo inayofanyika jijini Kampala, inalenga kuwasaidia wanawake kujenga taaluma katika mchezo wa soka na kuwavutia wachezaji wa kike, makocha, mameneja wa timu, waandishi wa habari na wasimamizi.

"Kwa karne nyingi, kandanda ulikuwa mchezo wa wanaume na sasa tunahitaji kuwawezesha wanawake," amesema mkuu wa uhusiano wa kimataifa wa UEFA Eva Pasquire .

Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA, linasema hili ni jaribio la makusudi la kuongeza idadi ya wanawake katika uongozi wa soka.

“Wakati wa mkutano wa  88 wa FUFA, tulikuwa na mwanamke mmoja au wawili, sasa tuna zaidi ya 10," amesema Moses Magogo rais wa FUFA.

Magogo ametoa wito kwa wanawake kuingia katika nafasi za maamuzi ikiwa wana lengo la kukua katika mchezo.

“Tumejaribu tangu 2013 kuendeleza soka la wanawake lakini changamoto zimekuwa za kitamaduni, kidini na zinazohusiana na wazazi.” ameongeza.

Hii ni ziara ya tatu kwa Pasquire nchini Uganda akiandaa Mijadala ya kuwasaidia wanawake walio kwenye soka.

Mtaalam wa masoko wa Uefa, Julia Anna Mcgeever na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake ya Saudi Arabia Monika Staab wamekua wakiandamana na kiongozi huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.