Pata taarifa kuu

Kenya,Tanzania na Uganda zawasilisha ombi la kuwa mwenyeji wa AFCON 2027

NAIROBI – Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limethibitisha kupokea ombi la pamoja kutoka nchi tatu za Afrika Mashariki, Kenya, Uganda na Tanzania, ambazo zinataka kuwa mwenyeji wa michuano ya bara Afrika AFCON mwaka 2027.

Kenya, Uganda na Tanzania zawasilisha ombi la pamoja kuwa mwenyeji wa AFCON 2027
Kenya, Uganda na Tanzania zawasilisha ombi la pamoja kuwa mwenyeji wa AFCON 2027 AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Michezo wa Kenya, Ababu Namwamba amesema amewasiliana na wenzake kutoka Tanzania na Uganda, na hivi karibuni kamati moja itaundwa kuendelea kushinikiza nafasi hiyo.

Iwapo ombi hilo litafanikiwa basi mashindano hayo yatarejea katika eneo la Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza baada ya miaka zaidi ya 50.

Mara ya mwisho mashindano hayo kufanyika katika ukanda huo ilikuwa ni mwaka 1976 wakati Ethiopia ilipokuwa mwenyeji.

Aidha, CAF inasema imepata maombi mengine kutoka Algeria, Botswana na Misri kutaka kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.