Pata taarifa kuu

La Liga ni ya wabaguzi wa rangi : Vinicius Junior

NAIROBI – Mchezaji wa Real Madrid Vinicius Junior amesema "La Liga ni ya wabaguzi wa rangi" baada ya kushambuliwa kwa maneno ya kibaguzi huko Valencia.

La Liga imesema itachunguza iwapo Vinicius Junior alibaguliwa kirangi
La Liga imesema itachunguza iwapo Vinicius Junior alibaguliwa kirangi AP - Alberto Saiz
Matangazo ya kibiashara

Vinicius Jr mwenye umri wa miaka 22 aliondolewa uwanjani kwa kufanya vurugu kwa dakika 97 baada ya kuzozana na Hugo Duro.

Kabla ya kuondolewa uwanjani, mchezaji huyo aliyeonekana kuwa na hasira, alijaribu kumfahamisha mwamuzi wa katikati kuhusu vitendo vya shabiki wa Valencia.

La Liga imesea kuwa itachunguza tukio hilo la kuchukua hatua za kisheria iwapo suala la matamshi ya kibaguzi yatapatikana katika uchunguzi wake. (AP Photo/Alberto Saiz)
La Liga imesea kuwa itachunguza tukio hilo la kuchukua hatua za kisheria iwapo suala la matamshi ya kibaguzi yatapatikana katika uchunguzi wake. (AP Photo/Alberto Saiz) AP - Alberto Saiz

Kupitia mtandao wake wa Instagram, raia huyo wa Brazil aliandika kuwa “michuano ambayo hapo awali ilikuwa ya Ronaldinho, Ronaldo, cristiano na Messi leo ni ya wabaguzi wa rangi,”.

Tukio hili halikuwa la kwanza, suala la ubaguzi wa rangi ni jambo ambalo limekuwa likishuhudiwa kwa sehemu kubwa kwenye, vitendo ambavyo hata wasimamizi wa ligi hiyo wanakiri kuwa la Kawaida.

Vinicius Junior, amekuwa akikabiliwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika Ligi ya La Liga kwa muda sasa
Vinicius Junior, amekuwa akikabiliwa na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika Ligi ya La Liga kwa muda sasa AP - Alberto Saiz

Katika taarifa yake, La Liga imesea kuwa itachunguza tukio hilo la kuchukua hatua za kisheria iwapo suala la matamshi ya kibaguzi yatapatikana katika uchunguzi wake, ikiwataka watu walio na ushahidi kutoa mikanda ya video kwa mamlaka.

Kupitia ukurasa wake wa twitter, rais wa, La Liga, Javier Tebas aliandika kuwa Vinicius mara mbili hakujitokeza kwenye mkutano wa kujadili nini kinachoweza kufanyika wakati ambapo visa vya kibaguzi vinatokea.

Vinicius kwa upanda wake alikashifu chapisho hilo kama lililokuwa linamlenga yeye kama mchezaji badala ya kuwalenga wabaguzi, akisema kwamba anataitaka La Liga kuchukua hatua na kuwaadhibu wahusika.

Mchezaji huyo amekuwa akilengwa na vitendo vya kibaguzi msimu huu.

Mechi hiyo kati ya Real Madrid dhidI ya Valencia ilisitishwa katika dakika 70 baada ya Vinicius kujaribu kuwazomea mashabiki waliokuwa wanamrushiwa maeneno ya kibaguzi.

Mchezaji wa  Real Madrid Vinicus alikabiliwa na vitendo vya kibaguzi wakati wa mechi yao dhidi ya Valencia, Mei 21, 2023.
Mchezaji wa Real Madrid Vinicus alikabiliwa na vitendo vya kibaguzi wakati wa mechi yao dhidi ya Valencia, Mei 21, 2023. REUTERS - PABLO MORANO

Baadae mchezaji huyo alitolewa nje ya uwanja kwa mara ya kwanza latika ligi ya La Liga kwa kukorofishana na wachezaji wa timu pinzani.

Kocha wa Real Madrid Ancelotti amekashifu kitendo hicho vikali akitaka hatua kuchukuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.