Pata taarifa kuu

Djokovic kuwania taji lake la 23 la Grand Slam

NAIROBI – Na Paul Nzioki

Novak Djokovic Mchezaji tennis raia wa Serbia
Novak Djokovic Mchezaji tennis raia wa Serbia AP - Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji wa tenisi Novak Djokovic atakua akiwania taji lake la 23 la Grand Slam akiwania pia kuvunja rekodi katika mashindano ya French Open.

Novak atashirikishi katika mashindano haya bila mpinzani wake wa zamani Rafael Nadal kwa mara ya kwanza tangu 2004.

Iga Swiatek mchezaji tennis kwa upande wa wanawake
Iga Swiatek mchezaji tennis kwa upande wa wanawake AP - Jim Rassol

Kwa upande wa kinadada Iga Swiatek atakuwa akilenga kuwa mwanamke wa kwanza kutetea taji hilo katika miaka 16 wakati ambapo michuano hiyo itaanza siku ya Jumapili.

Mkongwe wa Serbia Djokovic atakuwa kipenzi cha ubingwa, ingawa, amekua akisumbuliwa na jeraha la kiwiko cha mkono hadi kushindwa kufuzu robo fainali katika mechi zake tatu za uwanjani kufikia sasa msimu huu.

Holger Rune, Mchezaji wa tennis
Holger Rune, Mchezaji wa tennis AP - Thibault Camus

Wakati bingwa huyo akiwa nje ya uwanja, Carlos Alcaraz alishinda Barcelona na Madrid Open akiwa njiani kuchukua nafasi ya Djokovic kama mchezaji nambari moja ulimwenguni, huku Daniil Medvedev akiibuka wa pili kwa Roland Garros baada ya ushindi wake wa kwanza  huko Roma.

Raundi hii itakuwa wakati mwafaka kwa Djokovic kuwa mshindi mara 14 wa French Open na kumaliza katika kilele cha orodha ya muda wote wa mataji mengi ya wachezaji wa pekee kwenye Grand Slam.

rafael nadal
rafael nadal © Pierre René-Worms

Bingwa huyo mara mbili amepoteza mechi nane kati ya 10 za French Open na Nadal ambaye anakosa toleo la mwaka huu kutokana na jeraha la nyonga alilolipata kwenye michuano ya Australian Open.

 "Ninajua ninaweza kucheza vizuri zaidi kila wakati," Djokovic alisema baada ya kushindwa na Holger Rune katika mechi ya nane bora ya wazi ya Italia.

"Hakika ninatazamia kufanyia kazi vipengele mbalimbali vya mchezo wangu, wa mwili wangu, natumai nitajiweka katika umbo la asilimia 100. Hilo ndilo lengo.”

Djokovic na Alcaraz wamepangwa kukutana katika nusu fainali baada ya kuwekwa kwenye nusu ya droo hiyo.

Raia wa Serbia Novak Djokovic
Raia wa Serbia Novak Djokovic REUTERS - LOREN ELLIOTT

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 pia anaweza kulazimika kumpata bingwa wa Monte Carlo Masters Andrey Rublev katika robo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.