Pata taarifa kuu

Liverpool wakubali kumsajili Moises Caicedo kutoka Brighton

Nairobi – Liverpool wamekubali ada ya uhamisho wa rekodi ya Uingereza ya pauni milioni 110 kwa kiungo wa Brighton Moises Caicedo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari Ijumaa.

Liverpool wamekubali kumsajili Moises Caicedo kutoka Brighton
Liverpool wamekubali kumsajili Moises Caicedo kutoka Brighton AP - Kirsty Wigglesworth
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ecuador mwenye umri wa miaka 21 alikuwa akilengwa na Chelsea wakati wa kipindi cha uhamisho lakini  Brighton walikuwa wameshikiliwa kwamba mchezaji huyo hataondoka kwa chini ya pauni milioni 100.

Liverpool wamekuwa wakijenga upya safu yao ya kiungo baada ya kuondoka kwa Jordan Henderson na Fabinho.

Mchezaji pia alikuwa amehusishwa na klabu ya Chelsea
Mchezaji pia alikuwa amehusishwa na klabu ya Chelsea AP - Alastair Grant

Caicedo sasa atacheza na Alexis Mac Allister, mshindi wa Kombe la dunia la Argentina ambaye aliondoka Brighton na kuelekea Merseyside mwezi Juni.

Rekodi ya awali ya Uingereza ya pauni milioni 107 ilikuwa imeekwa na  Chelsea ambayo ililipa kwa Enzo Fernandez mwezi Januari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.