Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-MACHAR-SIASA

Riek Machar atarajiwa kuwasili Juba Jumatatu hii

Kiongozi wa waasi wa Sudani Kusini Riek Machar anatarajiwa kuwasili Jumatatu hii katika mji mkuu, wa Sudani Kusini, Juba, ambapo ataanza kuhudumu kama Makamu wa rais.

Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar, Kampala, Januari 26, 2016.
Kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini, Riek Machar, Kampala, Januari 26, 2016. SAAC KASAMANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ni muendelezo wa utekelezaji wa mkataba wa amani ambao mpaka sasa umeendelea kukiukwa na pande mbili husika katika mgogoro wa nchi hiyo.

Riek Machar anatazamiwa kuwasili mjini Juba Jumatatu hii mchana kwa mujibu wa msemaji wake Mabior Garang. Kurudi kwa kiongozi huyu wa waasi kunajenga matumaini ya kutatua vita vya wenyewe viliozuka mwezi Desemba 2013 na ambavyo vimesababisha maelfu ya watu kuuawa (idadi halisi haijulikani) na zaidi ya watu milioni 2.3 kukimbia makazi yao.

Mjini Juba, mabango yamewekwa sehemu mbalimbali yakitangaza kurudi kwa Riek Machar, na kuchukua nafasi yake zamani ya Makamu wa rais. Tayari alihudumu nafasi hii kati ya mwezi Julai 2011 - Siku ya Uhuru - na mwezi Julai 2013, wakati alitimuliwa kwenye nafasi hiyo na Rais Salva Kiir.

Salva Kiir alimteua mpinzani wake kwenye nafasi hii mwezi Februari 2016, na hivo kupelekea kuanzishwa kwa mkataba wa amani uliosainiwa Agosti 26, 2015, mkataba ambao ulitilia manani usitishwaji wa mapigano na utaratibu wa kugawana madaraka.

"Kupatanisha, kuunganisha taifa," hayo ni maneno ambayo yameandikwa kwenye mabango yaliyowekwa kwenye mtaa wenye vumbi wa mji mkuu, juu ya picha za viongozi hawa wawili wakitabasamu, ambao wanatazamiwa kuunda serikali ya mpito.

Kurudi kwa Riek Machar, ambaye hajaweka mguu wake katika mji wa Juba tangu kuanza kwa mgogoro nchini humo, kwanza ni ishara. Kwa sababu hatua ya utekelezaji kamili wa mkataba wa amani imekabiliwa na vikwazo.

- Juba katika hali ya taharuki-

kuwasili kwake "kutawawezesha kuundwa kwa serikali ya mpito, hatua muhimu katika utekelezaji wa mkataba wa amani," amesema Casie Copeland, wa shirika la kimataifa la kutatua migogoro (ICG), huku akionya kwamba hali hiyo haitomaliza mgogoro.

Licha ya kusaini makubaliano ya amani, mapigano hayajawahi kusimamishwa. Mapigano pia yanahusu makundi mengi ya waasi wakitetea hasa maslahi ya maeneo yao na ambao yanabaini kwamba hayahusiki na mikataba iliyoandikwa.

Katika mji wa Juba vile vile, mvutano umeibuka kabla ya wiki hii muhimu. Hofu inawachanganya raia kwa matumaini.

Askari hao wamegawanyika katika makambi mbalimbali yaliowekwa mji wa Juba na pembezoni mwake. Askari waliobaki, kutoka upande wa serikali na waasi, hawaruhusiwi kuingia katika eneo lenye umbali wa kilomita 25 karibu na mji mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.